Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki na Urusi wajadili mzozo kati ya Israel na Palestina. Picha: AA

Waziri Wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan na mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov walizungumza kwa njia ya simu na kujadili maendeleo katika mzozo kati ya Israeli na Palestina, vyanzo vya kidiplomasia vya Uturuki vilisema Jumatatu.

Siku kumi baada ya mgogoro na kundi la Palestina la Hamas, mashambulizi ya Israel na kuzingirwa kwa Gaza kumeendelea, huku zaidi ya watu milioni 1 ambao ni takriban nusu ya idadi ya watu wa Gaza wamefurushwa.

Gaza inakabiliwa na janga kubwa la kibinadamu huku watu wake wakikosa huduma ya umeme na maji safi na salama, huku kukiwa na uhaba mkubwa wa vyakula na vifaa vya matibabu. Idadi kubwa ya wakazi wa eneo hilo wameacha makazi yao kufuatia onyo la Israel la kuwataka waondoke maeneo ya kaskazini na kutishia kufanya mashambulizi.

Mapigano hayo yalizuka wakati Hamas ilipotekeleza Operesheni ya Mafuriko Ya Al-Aqsa Oktoba 7, shambulio la kushtua lenye pande nyingi ikiwa ni pamoja na mlipuko wa uzinduzi wa roketi na uingiliaji ndani ya Israeli kupitia ardhi, bahari na hewa.

Hamas ilisema uvamizi huo ulikuwa ni wa kulipiza kisasi kwa uvamizi wa msikiti wa Al-Aqsa na kuongezeka kwa vurugu za wahamiaj

Muda mfupi baadaye, Israeli ilizindua kile ilichokiita 'Operesheni ya Mapanga ya Chuma' dhidi ya maeneo ya Hamas ndani ya Ukanda wa Gaza.

Kufikia Jumatatu, Idadi ya Wapalestina waliouawa katika mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza imeongezeka na kufikia watu 2,750, wakiwemo watoto 750.

Wakati huo huo, kwa upande wa Israeli, watu 1,300 wameuawa.

AA