Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na mwenzake wa Algeria Abdelmadjid Tebboune wamekutana mjini Istanbul kwa mazungumzo.
Siku ya Jumamosi, Erdogan alimkaribisha Tebboune katika ikulu ya Dolmabahce, wakati rais wa Algeria alipoanza ziara yake ya kikazi ya siku mbili Uturuki siku ya Ijumaa.
Erdogan na Tebboune watafanya mazungumzo ya ana kwa ana na kufuatiwa na mikutano baina ya wajumbe.
Kiongozi wa Uturuki pia ataandaa chakula cha jioni kwa heshima ya wageni.
Masuala yote ya uhusiano kati ya Uturuki na Algeria na hatua za kuimarisha ushirikiano zitajadiliwa.
Masuala ya sasa ya kikanda na kimataifa pia yatakuwa kwenye ajenda.
Uturuki na Algeria zinajivunia historia ya pamoja na vile vile uhusiano wa kitamaduni uliokita mizizi.
Uhusiano wa nchi mbili umepata msukumo katika miaka iliyopita.
Nchi hizi mbili zilitia saini mkataba wa Urafiki na Ushirikiano mwaka 2006.