Mkutano huo, unaofanyika chini ya kauli mbiu "Sera Yetu ya Kigeni Katika Karne ya Uturuki," utaendelea hadi Agosti 9. Picha: AA      

Kongamano la 14 la kila mwaka la Mabalozi lilianza siku ya Jumamosi katika mji mkuu Ankara kwa kushirikisha mabalozi wa Uturuki wanaohudumu nyumbani na nje ya nchi.

Mabalozi hao pia watakuwa na fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu mienendo ya kimataifa ikiwemo fursa na changamoto za hivi majuzi kwani mkutano huo una jukumu muhimu la upangaji wa ndani wa sera za kigeni na uratibu wa taasisi.

Kama sehemu ya mkutano huo, Rais Recep Tayyip Erdogan atawapokea mabalozi hao ili kuwapa tathmini na miongozo ya sera za kigeni.

Spika wa Bunge Numan Kurtulmus pia anatarajiwa kukutana na mabalozi hao.

AA