By Hannah Ryder
Kuanzishwa upya kwa mkataba wa nafaka, ambao ulipatanishwa kwa mara ya kwanza na Uturuki na Umoja wa Mataifa mnamo Julai 2022, ni muhimu kwa vile unawezesha bidhaa - ikiwa ni pamoja na nafaka na mbolea - kutoka Ukraine kupitia eneo la Bahari Nyeusi hadi duniani kote, ikiwa ni pamoja na Afrika bara.
Mwezi mmoja kabla ya makubaliano ya awali, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Moussa Faki na Mwenyekiti wa wakati huo wa Umoja wa Afrika na Rais wa Jamhuri ya Senegal Macky Sall, walisafiri hadi Moscow kushinikiza amani na kujadili athari za vita dhidi ya Senegal eneo la Afrika.
Wawakilishi wakuu wa Umoja wa Afrika walifanya hivyo kwa mwongozo wa wakuu wa nchi za Afrika katika mkutano wa mapema Mei 2022.
Viongozi wa Kiafrika walikuwa wamegundua tatizo kwa sababu asili mia 8 ya jumla ya nafaka na asili mia 12 ya jumla ya mbolea barani Afrika hutoka Ukraine na Urusi, na vikwazo vyovyote vya usambazaji hatimaye vitasababisha mfumuko wa bei na hata uwezekano wa uhaba wa chakula.
Chaguo la Uturuki kuchukua suala hili, na kuifanya kuwa kipaumbele cha sera yake ya nje na kushirikiana na Urusi juu ya swali hili, bila shaka ilikuwa ngumu.
Uturuki kama mwanachama wa muungano wa NATO na nchi 20 zilizoendelea yaani G20, ilikuwa bado chini ya shinikizo kubwa la kuwekea Urusi vikwazo na kutarajiwa kutojihusisha na Urusi kwenye mada yoyote - huku hatua yoyote mbadala ikifasiriwa kama uidhinishaji wa vita.
Kusikiliza mitazamo ya Kiafrika
Hata hivyo, katika vikao vya kimataifa, Ankara imeweka wazi msimamo wake. Kwa mfano, Uturuki ameidhinisha mara kwa mara kura za baraza kuu la Umoja wa Mataifa kulaani Urusi kwa hatua zake zisizo halali katika ardhi ya Ukraine na dhidi ya watu wa Ukraine.
Walakini, kwa kuzingatia msukumo na mamlaka ya Kiafrika, uanachama wa Uturuki wa NATO na nchi za G20, pamoja na uhusiano wa karibu wa wakati mmoja na Urusi na kanda ya Afrika, uliipatia nchi hiyo nafasi ya kipekee katika maswala ya kigeni.
Serikali ya Uturuki kuwa tayari na kuwa na uwezo wa kusikiliza mitazamo ya Waafrika haukuibuka tu mnamo 2022. Uturuki ilizindua mkakati wake wa mahusiano na Afrika kwa mara ya kwanza mwaka 1998 na hadi sasa imeitisha mikutano mitatu ya Ushirikiano kati ya Uturuki na Afrika - mwaka 2008, 2014 na 2021.
Mkutano wa kwanza uliwasilisha Azimio la Istanbul na Mfumo wa Ushirikiano - ambao ulijumuisha maeneo mengi ya ushirikiano - kutoka kwa kilimo na biashara ya kilimo, huduma za afya, ushirikiano wa amani na usalama na hatua za ulinzi wa mazingira.
Mkutano wa pili ulipitisha Azimio la Malabo na mkutano wa Istanbul mnamo 2021 ulifikia kilele kwa azimio na mpango wa utekelezaji wa pamoja unaohusu amani, usalama na haki, 'maendeleo yanayozingatia binadamu' na 'ukuaji imara na endelevu'.
Kama mshirika wa maendeleo wa kanda, Uturuki imesisitiza mara kwa mara kwamba inazingatia msaada ambao hauhusiani na hali ya kisiasa au kiuchumi, inayotambua uhuru wa Afrika na kuonyesha nia ya kufanya kazi na nchi za Afrika kwa nia ya kuambatana na ajenda ya Umoja wa Afrika wa 2063 - mpango wa maendeleo ya pamoja wa Afrika kupitia miradi kumi na mitano.
Azimio la Malabo la mwaka 2014 lilirejelea kwa uwazi ajenda ya Umoja wa Afrika 2063 na kujumuisha miradi kama njia ya kutanguliza ushirikiano wa Uturuki na Afrika. Kwa hiyo, uhusiano wa kisiasa na kiuchumi kati ya Uturuki na bara umeendelea katika kipindi hiki.
Kiwango cha biashara cha Uturuki na Afrika kilifikia dola bilioni 25 mwaka 2020 - ikiwa ni ongezeko mara tano kutoka dola bilioni 5 mwaka 2000.
Serikali za Afrika zimeshirikisha wakandarasi na wafadhili wa Uturuki kujenga miradi 1,150 ya miundombinu yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 70.
Hii ni muhimu kutokana na upungufu wa miundombinu barani Afrika. Mpango mpya unaokaribishwa ni ujenzi wa Uturuki wa sehemu ya kilomita 368 ya reli inayogharimu dola bilioni 1.9 nchini Tanzania.
Na, labda cha kushangaza zaidi, hisa za uwekezaji wa sekta binafsi ya Uturuki barani Afrika zilifikia chini ya dola bilioni 2, mwaka 2019 ikiwa ni sehemu ya asili mia 3.5 ya ya uwekezaji kutoka nchi za nje ujumla .
Hii ni juu kuliko nchi zingine zilizoendelea ambazo zipo chini ya muungano wa G20 - na inaonekana kukua kwa kasi. Kuchangia kikamilifu ili kuhakikisha uthabiti katika kanda, kwa kuepuka changamoto za ugavi na mfumuko wa bei, kwa kuzingatia ajenda ya Kiafrika na kuuliza ni muhimu.
Hasa, ndivyo Ankara imefanya kwa kuamua kufanya upatanishi unaowajibika na kufanya hivyo kwa mafanikio.
Zaidi ya mpango wa Nafaka
Sasa inaonekana uwezekano kwamba bidhaa za kilimo za Urusi, muhimu kwa nchi nyingi za Afrika, zitaendelea kuhakikisha upatikanaji wa biashara na Afrika. Swali linabaki, kutokana na mafanikio haya, ni nini kinachofuata kwa Uturuki?
Je, Uturuki inaweza kuchangia vipi zaidi matarajio ya Afrika? Nje ya mpango wa nafaka, kuna hatua kadhaa zinazowezekana kwa Uturuki kuendelea kuleta vipaumbele vya maendeleo ya Afrika na sera za kigeni.
Fursa muhimu ya haraka kwa Uturuki ni kukubaliana kikamilifu na mwito mkali ambao ulitolewa na Rais Macky Sall kama Mwenyekiti wa AU mwaka wa 2022, kwa kanda ya Afrika kuwa na uwakilishi kamili katika muungano wa nchi za G20, kama vile umoja wa ulaya .
Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya tayari ni wanachama wa G20. Kuunga mkono kikamilifu na kwa uwazi msimamo huu wa haki kwa Afrika, kama vile Beijing na Washington tayari zimefanya, kungesaidia kuiingiza Afrika katika miundo ya sasa ya mahusiano ya kimataifa ya dunia.
Zaidi ya hayo, Uturuki kuvuta uzito wake kwa uwakilishi bora wa bara la Afrika kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa itakuwa na athari kubwa ya kisiasa na hatimaye kiuchumi.
Zaidi ya hayo, ugunduzi wa Uturuki unamaanisha kuongeza kwa uagizaji wa thamani ya ziada kutoka kwa bara na kuhimiza uwekezaji wa nje wa kijani na sekta ya kibinafsi inayohusiana na utengenezaji katika bara.
Hili ni muhimu hasa mwaka huu kwani viongozi wa Afrika wanaendelea na kazi yao ya kujaribu kuokoa bara kutokana na athari ya Uviko-19 na matatizo mengine ya ugavi, ikiwa ni pamoja na kuttimiza kauli mbiu ya mwaka ya Umoja wa Afrika kwa 2023 "Kuharakisha Utekelezaji wa bishara huru ndani ya Afrika".
Mwandishi, Hannah Ryder ni Mkurugenzi Mtendaji wa 'Development Reimagined', kampuni ya kimataifa ya ushauri wa maendeleo, na mwanadiplomasia na mwanauchumi wa zamani mwenye uzoefu wa miaka 20. Kanusho: Maoni yaliyotolewa na mwandishi hayawakilishi maoni na sera za uhariri za TRT Afrika