Kwa nini jina ‘Istanbul’ ni maarufi miongoni mwa kina dada nchini Somalia?

Shirika la TRT litawezesha desturi na tamaduni za watu wa Somalia kukua na kufahamika zaidi kupitia masomo ya utayarishaji filamu watakayoyatoa kwa watarishaji filamu. Tasnia ya filamu nchini Somalia ilikuwa na umaarufu mkubwa katika miaka ya nyuma lakini kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vikaharibu tasnia hio.

“Tumefanya mkutano na Wakurugenzi wa Shirika la TRT and watatusaidia pakubwa kurejesha desturi, muziki na filamu za watu wa Somali mahala pakee.” Msemaji wa Ikulu Abdirashid Mohamed Hashia aliambia shirika la habari la Anadolu.

Aidha Hashi aliongeza kuwa, “Filamu za Türkiye zitatafsiriwa kwa lugha ya Somali kwa lengo la kuhakikisha watu wa Somali vilevile wanazifahamu desturi za Turkiye.”

“Ukifanikiwa kwenda Turkiye na kuzuru Instanbul ama Ankara, utagundua jinsi gani watu wa kutokea Somalia waishio Türkiye wamekumbatiwa katika jamii ya Türkiye, wanafanya biashara na kusoma katika vyuo vikuu na hayo yote ni kutokana na hali halisi kuwa Shirika la ndege ya Türkiye linasafiri kwenda Mogadishu kila siku kusafirisha abiria.” Hashi aliongeza.

Somalia na Türkiye ziliimarisha uhusiano wa karibu mwaka 2011 kufuatia ziara ya Rais wa Türkiye Recep Tayyip Erdogan nchini humo, hii ikiwa ni ziara ya kwanza ya Rais kutoka nje ya Bara la Afrika kuzuru Somalia katika kipindi cha zaidi ya miaka 20.

“Filamu za Türkiye zimekuwa zikifuatiliwa sana nchini na kupelekea umaarufu wa filamu za mataifa mengine kudidimia. Awali watu wa Somalia walipenda kutazama filamu za Bollywood lakini hali hio sasa imebadilika.” Alisema Hashi.

Aidha hamu na uhitaji wa kuifahamu lugha ya Turkiye umeongezeka mara dufu mwaka huu miongoni mwa vijana hasa kina dada kutokana na Tasnia ya Filamu za Türkiye.

Zaynab Abdi Adan anapenda kutazama tamthilia za Turkiye. Anasema amekuwa akizifuatilia kwa miaka mitatu sasa na amejifunza lugha ya Türkiye.

“Napenda jinsi wanadhihirisha ukweli na ukakamavu inapokuja ni kwenye suala la mapenzi. Napenda sana. Sasa nimekuwa kama ‘mraibu’ wa tamthilia ya Alparslan; Bayuk Selcuklu, Mcheza-filamu naemkubali zaidi ni Alpagut.” Alieleza Zaynab.

‘Istanbul’

“Ukitaka kujua jinsi gani Türkiye ina ushawishi mkubwa hapa Somalia, chunguza tu juu ya majina mengi ya kina dada wa Somalia.” Alisema Mzee mmoja kwa jina Ahmed Osman. “Moja kati ya majina maarufu ya kike hapa Somalia ni ‘Istanbul,’ Alisema Ahmed. “Uhusiano wetu pia ni wa Kidini, na nafurahi kuona taifa kubwa la Kiislamu likiwa na ushawishi hapa kwa sababu miaka ya hapo nyuma palikuwepo na ushawishi wa magharibi kama vile desturi za Italia, lakini hali hiyo imebadilika.”

Sherehe maalum

Somalia mwaka huu iliadhimisha miaka 11 ya uhusiano na Türkiye. Wanadiplomasia wa kigeni, Viongozi Wakuu wa Somalia na Balozi wa Turkiye nchini Somalia ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria shereha za maadhimisho hayo Jijini Mogadishu. Wasanii wa Somalia na Türkiye walialikwa kuonesha kubadalishana/mwingiliano wa tamaduni na desturi za watu wa kutokea mataifa hayo mawaili.

AA