Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki / Picha: AA

Uturuki imepongeza uamuzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kuondoa vikwazo vya silaha dhidi ya Somalia.

"Tunatamani uamuzi huu wa kihistoria utaleta enzi mpya ambayo itapanda mbegu za amani, ustawi na matumaini makubwa kwa mustakabali wa Somalia," wizara ya mambo ya nje ilisema katika taarifa.

Pia iliongeza kuwa Ankara " kama kawaida, itaendelea kusimama na watu wa Somalia na kuunga mkono Somalia katika enzi hii mpya."

Taarifa hiyo inajiri baada ya siku ya Ijumaa, Baraza la Usalama, kwa kauli moja, kupiga kura ya kuondoa vikwazo vya muda mrefu vya kupeleka silaha kwa serikali ya Somalia na vikosi vyake vya usalama.

Baraza la Usalama liliweka marufuku ya jumla na kamili ya silaha dhidi ya Somalia kwa mara ya kwanza mnamo 1992 kufuatia mzozo wa wakati huo na kuzorota kwa hali ya kibinadamu nchini humo.

AA