Kundi la Kituruki linashinikiza watu ulimwenguni kote kuwasha na kuzima taa zao kwa wakati mmoja -saa tatu usiku- Jumatatu, (kwa saa za kwao nyumbani) na kila usiku baada ya hapo , kwa kampeni ya "Fanya Kitu" kusaidia watoto waliozingirwa wa Gaza.
Jumatatu ni siku ya 44 ya mashambulizi ya Israel huko Gaza, huku zaidi ya raia 13,000 wa Palestina, wakiwemo maelfu ya watoto na watoto wachanga, wakiuawa katika mashambulizi ya Israel ambayo wengi wanayaita uhalifu wa kivita, lilisema Jukwaa la Mshikamano la Ankara, kundi lililoandaa maandamano hayo.
Mnamo Novemba 20, Siku ya Watoto Duniani, kampeni ya uhamasishaji ilizinduliwa na kauli mbiu "Fanya Kitu," huku kampeni ikipangwa kuendelea hadi kusitishwa "mauaji ya watoto" yanayofanywa na Israeli.
''Kwa tukio la kwanza la kampeni, kuwasha na kuzima taa saa 9 usiku kwa saa za huko katika kila nchi kumepangwa kufanywa kote ulimwenguni,'' ilisema.
Katika siku zijazo, jukwaa linalenga kuongeza uelewa wa umma wa kimataifa na upinzani wa kimataifa dhidi ya vifo vya watoto kupitia shughuli kama hizo.
Maudhui na nyenzo za kuona zitakazozalishwa wakati wa kampeni ya "Fanya Kitu" zitashirikiwa kwenye mitandao ya kijamii na lebo za #dosomething na #birseyyap kwa Kituruki, lilisema kundi hilo.