Kiongozi wa kundi la kigaidi la FETO Fetullah Gulen afariki nchini Marekani

Kiongozi wa kundi la kigaidi la FETO Fetullah Gulen afariki nchini Marekani

Kiongozi huyo wa FETO amekuwa akijificha katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani kwa miaka mingi.
Gulen, mkuu wa Shirika la Kigaidi la Fetullah (FETO), alisimamia mtandao mkubwa wa kigaidi unaolenga kudhoofisha serikali ya Uturuki na demokrasia. / Picha: Jalada la AA

Fetullah Gulen, ambaye ndiye aliongoza jaribio la mapinduzi ya mwaka 2016 nchini Uturuki, amefariki katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani, kulingana na ripoti. Alikuwa na umri wa miaka 83.

Herkul, tovuti ya propaganda ya kundi la kigaidi, ilisema kupitia mtandao wake ya X kwamba Gulen alifariki Jumapili jioni katika hospitali alikokuwa akitibiwa.

Kwa miongo kadhaa, Gulen, mkuu wa Shirika la Kigaidi la Fetullah (FETO), alisimamia mtandao mkubwa wa ugaidi unaolenga kudhoofisha serikali ya Uturuki na demokrasia.

Gulen alikuwa akiishi katika jimbo la Pennsylvania la Marekani. Viongozi wa Uturuki kwa muda mrefu walitaka arejeshwe, lakini maafisa wa mahakama wa Marekani hawakuidhinisha.

FETO na kiongozi wake anayeishi Marekani Fethullah Gulen waliandaa mapinduzi yaliyoshindwa ya Julai 15, 2016, nchini Uturuki ambapo watu 252 waliuawa na 2,734 kujeruhiwa.

Ankara pia inaishutumu FETO kwa kuwa nyuma ya kampeni ya muda mrefu ya kupindua serikali kwa kupenya katika taasisi za Uturuki, haswa jeshi, polisi na mahakama.

TRT World