"Haijalishi wanachofanya (Israeli), wanahukumiwa mbele ya ubinadamu na siku moja watawajibika mbele ya sheria," Celik aliongeza. / Picha: AA

Kampeni ya Israel ya kumkashifu Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan si kitu bali ni jaribio la kuficha ukatili wa Israel dhidi ya Wapalestina maeneo ya Gaza, Naibu Mwenyekiti na Msemaji wa Chama cha AK, Omer Celik, amesema.

"Tamko kali la waziri wa mambo ya nje wa Israel kumlenga rais wetu si lolote ila ni juhudi za kuficha mauaji yaliyofanywa na serikali ya Israel," Celik aliandika kwenye mtandao wa X siku ya Jumamosi.

Maoni hayo yalikuja kufuatia post ya mwanadiplomasia mkuu wa Tel Aviv Israel Katz kupitia mtandao wa X, ambapo alionesha picha ya Erdogan na Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas Ismail Haniya wakipeana mikono wakati wa ziara ya mkuu wa Hamas Istanbul, akisema kiongozi wa Uturuki "hana aibu".

"Muslim Brotherhood: Ubakaji, mauaji, unajisi wa maiti, kuchoma watoto wadogo," Katz aliandika.

"Wauaji watoto wanachukia mpango wowote wa kusitisha mashambulizi na mchakato wa amani. Sera inayoongozwa na rais wetu ya kusitisha mapigano na amani inalengwa na mitandao hii ya mauaji kwa sababu hiyo," Celik alijibu.

"Lakini bila kujali wanachofanya (Israeli), wanahukumiwa mbele ya haki na siku moja watawajibika mbele ya sheria," aliongeza.

Zaidi ya watoto 14,000 waliuawa na Israeli

Ikipuuza uamuzi wa muda wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki, Israel inaendelea na mashambulizi yake dhidi ya Gaza, ambapo Wapalestina wasiopungua 34,049 wameuawa, na 76,901 kujeruhiwa tangu Oktoba 7, kulingana na mamlaka ya afya ya Palestina.

Zaidi ya watu 14,000 waliouawa na mashambulizi ya Israel ni watoto.

Israel inashutumiwa kwa mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki. Uamuzi wa muda wa mwezi Januari uliiamuru Tel Aviv kusitisha vitendo vya mauaji ya halaiki na kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba msaada wa kibinadamu unatolewa kwa raia huko Gaza.

Uhasama umeendelea bila kuisha, hata hivyo, utoaji wa misaada bado hautoshi kushughulikia janga la kibinadamu.

TRT World