Fidan ameelezea nia yake ya kuitisha vikao vya aina hiyo ili kukuza ushirikiano/ Picha: AA  

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan amesisitiza nia 'isiyoyumba' ya Uturuki katika kuisaidia Bosnia na Herzegovina, kufikia uhuru na umoja.

“Msimamo wetu uko wazi kwa pande zote nchini Bosnia na katika ukanda mzima. Kwa mara nyingine tena, nathibitisha uungaji mkono wetu kwa umoja wa Bosnia Herzegovina,” alisema Fidan katika mkutano na waandishi wa habari na mawaziri wenzake wa Bosnia na Croatia katika mji wa Dubrovnik ulioko Croatia siku ya Jumamosi.

Akisisitiza kuwa Bosnia na Croatia ni wa muhimu kwa ajili ya amani ya Bosnia na kanda nzima, Fidan alisema kuwa walijadiliana masuala tofauti ikiwemo hali ya kisiasa Bosnia.

“Ni matumaini yetu kuwa miradi hii itachangia maendeleo ya uchumi wa kanda yetu,” aliongeza.

Akielezea wasiwasi wa Ankara kufuatia matamshi na vitendo vya mgawanyiko vinavyoendelea nchini Bosnia, Fidan amesisitiza umuhimu wa kuunda mazingira ya upatanishi.

"Pia, tuligusia suala la kuunganisha miradi ya miundombinu huko Bosnia na Croatia," aliongeza.

Akibainisha mafanikio ya kikao hicho, Fidan alisisitiza haja ya kuitisha mikutano ya aina hiyo mara kwa mara kwa lengo la kukuza ushirikiano.

Ushauri wa pande tatu

Fidan na Waziri wa Mambo ya Nje wa Albania Igli Hasani walikutana katika mji wa Croatia wa Dubrovnik kando ya mkutano wa Uturuki-Bosnia na Herzegovina-Croatia, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ilisema katika mtandao wa X, siku ya Jumamosi.

Kufuatia kikao chake na Hasani, Fidan alikutana pia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Bosnia na Herzegovina Elmedin Konakovic.

Baada ya kukutana na Konakovic, Fidan pia alipata wasaa wa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Croatia Gordan Grlic Radman.

Fidan yuko Croatia akishiriki mkutano wa Jumamosi wa utaratibu wa ushauri wa pande tatu unaohusisha Uturuki na mataifa ya Balkan.

Pia, atafanya mazungumzo ya nchi mbili, kando ya mkutano huo, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki.

TRT Afrika