Uturuki ilishuhudia mapinduzi yake ya umwagaji damu zaidi katika nyakati za hivi karibuni mnamo Julai 15 2016 wakati wanachama waasi wa jeshi na vikosi vya usalama walijaribu kuipindua serikali ya Rais Recep Tayyip Erdogan iliyochaguliwa kidemokrasia.
Mashambulizi ya anga yalilenga bunge katika mji mkuu Ankara huku wanajeshi wakivamia makao makuu ya chama tawala cha AK na kumshika mateka Mkuu wa Majeshi Jenerali Hulusi Akar.
Huku milio ya risasi na milipuko ikitanda katika miji ya Ankara na Istanbul hadi usiku, raia wa kawaida waliingia mitaani kupinga mapinduzi - wengine kujirusha mbele ya vifaru vilivyokuwa vikizurura mitaani.
Zaidi ya watu 250 waliuawa na wengine zaidi ya 2,000 kujeruhiwa.
Mamlaka ilimtaja Fetullah Gulen na shirika lake la ugaidi, Shirika la Kigaidi la Fethullah (FETO), kama washukiwa wakuu wa jaribio la mapinduzi. Maelfu ya wanaotuhumiwa kuhusika walitoroka Uturuki katika saa na siku zilizofuata mapinduzi, huku wengi wao wakiishia nchi za Ulaya.
Kampeni ya miongo kadhaa
Mamlaka ya Uturuki inasema ni njama kali iliyokuwepo kwa miongo kadhaa nchini. Kabla ya mapinduzi, ilijaribu kushawishi hali ya kisiasa nchini kwa kujipenyeza kwenye kiini cha taasisi za serikali, kwa mujibu wa maafisa wa Uturuki.
Fetullah Gulen, ambaye anaongoza kundi la ugaidi, amekuwa akiishi kwa kupewa ulinzi katika jimbo la Pennsylvania la Marekani. Anatuhumiwa kuendesha kampeni ya miongo kadhaa ya kupindua serikali ya Uturuki.
Gulen alianza harakati katika miaka ya 1960 kama kiongozi wa kidini na kujihusisha na siasa za Uturuki na anaaminiwa kuweka msingi wa shirika ambalo lilikuja kusambaa kote duniani.
Wakosoaji wanasema yeye alifanya hivyo hasa kwa kufungua shule zilizotimiza dhamira ya kijasusi yenye mitandao nje ya nchi - kutoka Marekani hadi Asia ya Kati, Afrika na Ulaya.
Hata hivyo, athari za shirika hilo la kigaidi zimepungua katika nchi nyingi tangu mapinduzi hayo yaliyofeli huku watu wakijitenga nalo.
‘’Mfano mashuleni, ungeweza kuona idadi kubwa ya wafanyakazi wa kitaaluma na wasio wa kitaaluma wakiwa raia wa Uturuki lakini kufuatia matukio tangu 2016, idadi hiyo imepungua. Katika hospitali pia idadi hiyo imepungua,’’ Kabiru Adamu, mkuu wa kampuni ya ushauri wa usalama ya Beacon Consulting ya Afrika Magharibi inaambia TRT Afrika.
Kuvunja mtandao
Shule za FETO zimetumika na kujulikana kama mahali ambapo damu mpya, kwa madhumuni yao ya kifisadi walishawishiwa kuingia kwanza kwa kisingizio cha mazungumzo ya kidini na kisha kuwateua watu ambao wangewekwa kisiri katika jeshi la taifa, mahakama na idara ya polisi.
Baadhi ya wafanyabiashara wakuu na maprofesa wa vyuo pia walishurutishwa kushirikiana au kwa hiari yao wenyewe walijihusisha na kundi hilo.
Ulikuwa mkakati wa kuwaajiri watu kinyume cha sheria ambapo waliwageuza vijana waliohitimu vyuo kuwa rasli mali zao muhimu kwa njia ya kuwapotosha kiitikadi.
Kufuatia jaribio la mapinduzi, kulikuwa na makubaliano kati ya serikali ua Uturuki na upande wa upinzani kuwa shirika linapaswa kushughulikiwa mara moja.
Serikali imekuwa ikisambaratisha mtandao wa FETO ndani ya nchi na vile vile kujaribu kushawishi serikali za kigeni kote duniani kukandamiza shughuli za shirika hilo katika maeneo yao.
Ndani ya Uturuki, wanachama wa shirika la kigaidi la Gulenist waliondolewa kutoka kwa taasisi zote za utawala, haswa katika vyombo vya kijeshi na usalama. Baadhi ya watu mashuhuri na taasisi zilizo na uhusiano wowote na shirika hilo zimeonekana wazi kuondolewa.
Serikali pia ilifunga zaidi ya mashule 1,000 zinazohusishwa na Gulen ndani ya Uturuki na kutoa wito kwa mataifa mengine washirika kuchukua hatua sawa dhidi taasisi zozote za kundi hilo.
Maafisa wa usalama wa Uturuki pia wamewakamata maafisa wa vyeo vya juu katika shirika la FETO- walioko nje ya nchi na kuwarejesha Uturuki kufunguliwa mashitaka.
Kwa mfano, mnamo 2021, Selahaddin Gulen - mpwa wake Fethullah Gulen - alikamatwa nchini Kenya katika operesheni ya shirika la kijasusi la kitaifa la Uturuki, MIT.
Alikuwa anatafutwa kwa tuhuma za kuwa mwanachama wa shirika la kigaidi.
Kwa miaka mingi, Uturuki imekuwa ikijaribu kushinikiza Fetullah Gulen kuhamishwa kutoka Marekani
Pia inataka kuwarejesha washukiwa kutoka nchi nyingine 27.
Kumekuwa na mabadiliko kwa mtazamo wa washirika wa Uturuki wa kidiplomasia kuona mtandao wa shirika la Gulen kama kundi la kigaidi.
FETO barani Afrika
Shirika la kigaidi la Gulen linaendesha mtandao wa kimataifa wa taasisi za elimu kote ulimwenguni. Na huku zile za Uturuki zimefungwa, bado kuna mamia ya shule zinazohusishwa na FETO zinazofanya kazi kote ulimwenguni ikiwa ni pamoja na Afrika.
Shule hizo zinazingatiwa kama vyanzo vya ufadhili ya shirika hilo . Mamlaka ya Uturuki imefanikiwa kushawishi serikali kadhaa barani Afrika kusitisha shule ambazo zinamilikiwa na shirika hilo . Hii imefanyika in Sudan, Guinea, Mali, Somalia, Mauritania, Niger, Chad, Tunisia and Senegal.
Shule hizi zimefungwa na zingine kukabidhiwa Maarif Foundation, taasisi iliyoundwa na serikali ya Uturuki kushughulikia masuala ya elimu ya kimataifa ikiwa ni pamoja na programu za ufadhili wa masomo.
Lakini Uturuki pia imekuwa na changamoto za kushawishi baadhi ya nchi nyingine za Kiafrika, kusitisha shughuli za biashara zinazohusishwa na FETO. Baadhi ya wachambuzi wanasema FETO pia ilijaribu kuficha baadhi ya shughuli zake.
"Baadhi yao walibadilisha umiliki wao, wengine walibadilisha jina kwa sura yao ya nje na kisha majina yao. Kwa hivyo ilikuwa vigumu kwa mfano kudai na kudumisha mantiki kwamba yanahusishwa na Fetullah," mchambuzi wa usalama Kabiru Adamu anasema.
Ingawa Uturuki bado haijafanikiwa kwa asilimia 100 dhidi ya FETO, nje ya nchi, juhudi za kidiplomasia ''imefaulu kupunguza ushawishi wa kundi hilo,'' anaongeza.