Rais Recep Tayyip Erdogan na rais Vladimir Putin wamejadili maendeleo ya hivi punde nchini Urusi kwa njia ya simu. / Picha: AA 

Rais wa Uturuki, katika mazungumzo ya simu na mwenzake wa Urusi, ameelezea kuwa Uturuki iko tayari kuchangia kwa utatuzi wa amani wa matukio nchini Urusi haraka iwezekanavyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumamosi na idara ya mawasiliano ya Uturuki, Recep Tayyip Erdogan na Vladimir Putin walijadili matukio ya hivi punde nchini Urusi baada ya kikundi cha Wagner kuanzisha uasi wa kutumia silaha dhidi ya serikali ya Urusi.

Katika maongezi yao ya simu, Erdogan alisisitiza umuhimu wa kutenda kwa kutumia maarifa.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa "hakuna mtu anayepaswa kujifanyia maamuzi juu kuhusu kukabiliana na hali nchini Urusi."

"Kwa maana hii, sisi kama Uturuki tuko tayari kufanya wajibu wetu ili matukio hayo yatatuliwe kwa utulivu na amani," Erdogan alisema, kulingana na taarifa hiyo.

Mamluki wa Wagner katika uasi mpya dhidi ya Putin

Prigozhin alishutumu vikosi vya Urusi kwa kushambulia wapiganaji wake, madai ambayo Moscow inakanusha.

Prigozhin, katika miezi ya hivi karibuni, ameishutumu mara kwa mara wizara ya ulinzi ya Urusi na waziri wa ulinzi Sergei Shoigu kwa kutosambaza silaha za kutosha kwa kundi lao.

Wagner wamekuwa akipigana pamoja na jeshi la Urusi nchini Ukraine.

TRT Afrika