Erdogan anatarajiwa kufanya mkutano wa ushirikiano na Waziri Mkuu Sharif Alhamisi. / Picha: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amewasili Pakistan katika ziara ambayo taifa hilo linasema "itaimarisha undugu na kuchagiza ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili."

Erdogan alipokelewa Jumatano jioni katika Uwanja wa ndege Nur Khan katika mji mkuu Islamabad na ujumbe wa maafisa wa Pakistani, akiwemo Rais Asif Ali Zardari na Waziri Mkuu Shehbaz Sharif.

Kwenye ujumbe wa Rais wa Uturuki yuko mke wa Rais Emine Erdogan, Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan, Waziri wa Ulinzi Yasar Guler, na Mkurugenzi wa Mawasiliano Fahrettin Altun.

Erdogan anatarajiwa kufanya mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu Sharif Alhamisi na pia kuhudhuria Mkutano wa 7 wa ngazi ya juu wa baraza la mkakati wa mataifa hayo mawili (HLSCC).

"Baada ya kukamilisha kikao, tutatoa tamko la pamoja na kutia saini makubaliano kadhaa. Viongozi hao wawili pia watazungumza na waandishi wa habari ," Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan ilisema.

"Pakistan na Uturuki wana ushirikiano wa kihistoria. Ziara hii ya Rais wa Uturuki na kushiriki kwenye mkutano wa 7 wa HLSCC utaimarisha undugu na uhusiano katika maeneo mbalimbali baina ya mataifa haya mawili ."

Masuala ya ushirikiano na kikanda

Erdogan pia anatarajiwa kuhudhuria hafla inayojumuisha wafanyabiashara wa Uturuki na Pakistan pamoja na kufanya mkutano kuhusu ushirikiano na Zardari katika ofisi ya rais.

HLSCC ni kikao cha ngazi ya juu kinachotoa maamuzi, na kutoa dira ya mikakati ili kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Kuna kamati kadhaa chini ya usimamizi wa HLSCC, zikijumuisha masuala ya biashara, uwekezaji, benki, fedha, utamaduni, utalii, nishati, ulinzi, kilimo, uchukuzi, mawasiliano,teknohama, afya, sayansi na teknolojia na elimu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan ilisema.

Kuunga mkono wa Uturuko katika suala la Palestina na Kashmir kunawiana na sera ya mambo ya nje ya Pakistan.

Viongozi wa nchi zote mbili wanatarajiwa kujadili masuala ya kikanda pamoja na vita vya Israeli vilivyosababisha mauaji ya halaiki Gaza.

TRT World