Rais wa Uturuki amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na mashirika ya haki za kibinadamu kuchukua hatua za haraka. /Picha: AA  

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amelaani vikali mashambulizi ya Israeli nchini Lebanon, akiituhumu Tel Aviv kwa kuendeleza 'mauaji ya kimbari' kuelekea Lebanon.

"Matokeo yake, raia wengi, wakiwemo watoto wameuwawa ndani ya wiki iliyopita kutokana na mashambulizi ya Israeli," alisema Rais wa Uturuki kupitia mtandao wa X, siku ya Jumamosi.

“Hakuna mtu yeyote yule mwenye dhamira njema ataridhia mauaji haya,” alisema Erdogan akiongeza kuwa, Israeli, ikiwa inajificha katika kivuli cha kuungwa kimataifa kwa kupewa silaha, inadharau utu, tunu za kibinadamu na sheria ya kimataifa.

Rais wa Uturuki amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na mashirika ya haki za kibinadamu kuchukua hatua za haraka.

Pia, ameweka msisitizo katika haja ya ulimwengu wa Kiislamu kuonesha msimamo dhidi ya mashambulizi hayo.

Mshikamano wa Uturuki kwa Lebanon

"Lazima kuwepo kwa kusitishwa kwa nguvu kwa majaribio ya Israeli ya kueneza sera zake za vurugu, ambazo zimetekelezwa huko Gaza na Ramallah, Lebanon maeneo mengine ya kikanda."

Akisisitiza mshikamano wa Uturuki kwa Lebanon, Erdogan alisema kuwa nchi yake itaendelea kusimama na watu wa Lebanon na serikali yao wakati wa kipindi hiki cha changamoto.

Alimalizia kwa kutoa salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao, na kuwatakia afueni ya haraka majeruhi wote.

Jumla ya watu 783 wameuawa na takriban 2,312 kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga ya Israel huko Lebanon tangu Septemba 23, na kufanya idadi ya vifo tangu Oktoba iliyopita hadi 1,622, na watu 5,549 wamejeruhiwa, kulingana na vyanzo rasmi vya Lebanon.

Mashambulio ya mabomu ya Israeli pia yamesababisha watu 98,800 kuyahama makazi yao, kwa mujibu wa Kitengo cha Kudhibiti Hatari za Maafa cha serikali ya Lebanon.

TRT Afrika