Ushindi wa Lyon dhidi ya Monaco Jumapili uliwapa Kylian Mbappé na wenzake uongozi wa pointi 12. / Picha: AFP

PSG wameshinda mataji 10 kati ya 12 ndani ya misimu 12 iliyopita, rekodi inayonyesha jinsi uwekezaji wa Qatar wa klabu hiyo, 2011 umewabadilisha kabisa na uso wa soka Ufaransa kwa ujumla.

Ingawa PSG ingeshinda taji hilo Jumamosi kwa ushindi nyumbani dhidi ya Le Havre, walitoka sare 3-3.

Ushindi wa Lyon dhidi ya Monaco Jumapili uliwapa Kylian Mbappé na wenzake uongozi wa pointi 12 na ubingwa wa rekodi ya Ufaransa wa mara ya 12 zikiwa zimesalia mechi tatu.

Kufungwa kwa Monaco na Lyon uliwapa taji PSG rasmi, na kuwaandaa kwa mechi ya mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa ya Jumatano ugenini dhidi ya Borussia Dortmund nchini Ujerumani.

PSG wapo mbioni kuinua mataji matatu msimu huu, huku fainali ya kombe la Ufaransa dhidi ya Lyon itakayochezwa Mei 25, baada ya kushinda kombe la Mabingwa wa Ufaransa.

Klabu hiyo ya Luis Enrique pia inatarajia kuifunga Dortmund na kutua fainali ya Ligi ya Mabingwa, Juni 1.

AFP