Oscar Pistorius to leave prison

Nyota wa Olimpiki wa Walemavu wa Afrika Kusini aliyefungwa jela Oscar Pistorius alipewa msamaha siku ya Ijumaa zaidi ya miaka 10 baada ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp, ​​na ataachiliwa mnamo Januari 5, mamlaka ilisema.

Pistorius - anayejulikana kama "Blade Runner" kwa miguu yake bandia ya nyuzi kaboni - alimpiga risasi mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 29 na mhitimu wa sheria kupitia mlango wa bafuni katika Siku ya Wapendanao mwaka 2013, na baadaye aliambia mahakama mara kwa mara kwamba alimkosea kama mvamizi.

Wakili wa familia ya Steenkamps alisema siku ya Ijumaa hawakushangazwa na uamuzi wa msamaha wa mapema (Parole) , uliotolewa baada ya Pistorius kukamilisha sehemu maalum ya kifungo chake.

'Nilikuwa nimekusamehe kitambo' - mama yake muathiriwa

Lakini katika kuelekea kusikilizwa kwa kesi siku ya Ijumaa, mamake Reeva Steenkamp June alitoa taarifa akisema haamini kuwa Pistorius alikuwa 'amerekebishwa tabia.'

Oscar Pistorius

"Urekebishaji tabia unahitaji mtu kujihusisha kwa uaminifu na ukweli kamili wa uhalifu wake na matokeo yake," taarifa yake ilisoma.

Alisema alikuwa amemsamehe "muda mrefu uliopita kwani nilijua hakika kwamba singeweza kuishi ikiwa ningeshikilia hasira yangu," aliongeza bi Steenkamp.

Lakini Mahakama ya Juu ya Rufaa mwishoni mwa 2015 ilimpata na hatia ya shtaka kubwa zaidi la mauaji baada ya rufaa ya waendesha mashtaka.

Alifungwa jela miaka sita mwaka wa 2016, chini ya nusu ya hukumu ya chini zaidi ya miaka 15 iliyokuwa ikiitishwa na waendesha mashtaka.

Lakini mwaka uliofuatia 2017, Mahakama ya Juu iliongeza zaidi ya mara mbili kifungo chake hadi miaka 13 na miezi mitano, ikisema kifungo cha miaka sita gerezani kilikuwa "kidogo cha kushangaza".

''Pistorius atamaliza kifungo kilichosalia katika mfumo wa marekebisho ya jamii na atasimamiwa kwa kufuata masharti ya parole hadi kifungo chake kitakapoisha,” Idara ya Huduma za Urekebishaji ilisema Ijumaa.

Vigezo gani vinamwezesha mtu kuachiliwa mapema gerezani?

Pistorius, ambaye alifikisha umri wa miaka 37 wiki hii, atalazimika kuendelea na matibabu ya kudhibiti hasira kama sharti la msamaha wake, wakili wa familia ya Steenkamp Tania Koen alisema.

Sababu kadhaa kwa kawaida huzingatiwa na bodi ya parole, ikiwa ni pamoja na asili ya uhalifu, uwezekano wa kukosea tena, mwenendo gerezani, ustawi wa kimwili na kiakili na vitisho vinavyoweza kumkabili mfungwa akiachiliwa.

Pistorius alikataliwa ombi lake kuachiliwa mapema mwezi Machi baada ya kuamuliwa kuwa hajamaliza muda wa chini wa kizuizini unaohitajika kuzingatiwa kwa msamaha.

Hata hivyo, Mahakama ya Katiba ilisema mwezi Oktoba kuwa Pistorius alikuwa ametumikia nusu ya kifungo chake kufikia Machi 21, jambo ambalo lilimaanisha kuwa anastahili, baada ya hukumu yake kuhesabiwa kutoka nyuma Julai 2016 badala ya Novemba 2017.

Reuters