Bafana Bafana ya Afrika Kusini hawakuwa wanashikika walipoilaza Namibia 4-0 katika mchezo wao wa pili wa kundi E, la TotalEnergies CAF Kombe la Mataifa ya Afrika Côte d'Ivoire 2023 dhidi ya Namibia Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly huko Korhogo.
Afrika Kusini ilianza wa kutia presha tangu mwanzo wa mchezo na kutengeneza nafasi katika hatua za awali za mchezo.
Presha hiyo ilizaa matokeo katika dakika 9 tu ya mchezo huku mpira ukigonga mikono ya beki wa Namibia kwa penalti. Uamuzi huo ulipuuzwa awali lakini baada ya kushauriana na VAR, Mwamuzi Youcef Gamouh aliruhusu bao hilo.
Percy Tau alijitokeza tena lakini akaiweka sawa wakati huu kwa Afrika Kusini kutoka papo hapo. Hakumpa nafasi kipa Lloyd Junior Kazapua alipopiga mpira kwenye kona ya chini ya kulia ya wavu dakika ya 14.
Afrika Kusini iliongeza idadi yao dakika 9 baadaye. Thapelo Morena alionyesha ustadi mkubwa baada ya kumpata Themba Zwane na pasi na kumalizia lango la timu kubwa kwa shuti kali upande wa kulia wa lango.
Zikiwa zimesalia dakika 5 kipindi cha kwanza kumalizika, Themba Zwane alifunga mabao 3-0. Wakati huu, ilikuwa ni juhudi ya pekee kutoka kwa fowadi huyo ambaye alipiga chenga kwenye safu ya ulinzi ya Namibia na kufunga bao.
Kufikia mapumziko Bafana walikuwa wanaongoza 3-0. Ungedhani kuwa watakuja wametulia lakini wapi! ndio mwanzo walirudi nusu ya pili kwa mikiki wakishambulia baada ya shambulio.
Thapelo Maseko aliongeza bao la nne baada ya kumwacha kipa Lloyd Junior Kazapua akiwa hoi kwa juhudi zake ambazo ziliishia kimiani.
Kundi E linaongozwa na Mali, huku Afrika Kusini ikishikilia nafasi ya pili pamoja na Namibia kwa pointi 3 na Tunisia wakiwa chini kwa pointi moja.
Afrika Kusini itacheza na Tunisia katika mechi yao ijayo ikiwa ndio ya mwisho ya makundi kwenye Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly mjini Korhogo Jumatano, Januari 24 wakiwa na matumaini ya kufuzu.