Nahodha wa Argentina Lionel Messi, ambaye ameondoka Ulaya kwenda kuichezea Inter Miami, baada ya kuisaidia Argentina kushinda Kombe la Dunia, atawania tuzo hiyo dhidi ya wachezaji wa Manchester City Kevin De Bruyne na Erling Haaland ambao walisaidia City kushinda taji la Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.
Hata hivyo, tofauti na Haaland na De Bruyne, Messi tayari ameshinda tuzo ya UEFA mara mbili katika historia yake ya miaka 12, haswa katika miaka ambayo Barcelona ilikuwa bingwa wa Ulaya.
Ingawa Messi aliichezea Paris na kumaliza msimu na taji lake la pili la Ligue 1, ni ushujaa wake kwenye Kombe la Dunia la FIFA akiwa na Argentina ndio uliwavutia wengi.
Nyota wa kizazi chake, Messi amekuwa Muargentina wa kwanza kubeba Kombe la Dunia tangu Diego Maradona, huku akifunga mabao saba katika mchakato huo alipotunukiwa Mpira wa Dhahabu kwa mchezaji bora wa jumla kwenye fainali. Mnamo Machi, alikua mchezaji wa tatu tu katika historia kufikisha mabao 100 ya kimataifa.
Kwa upande wake, Kevin De Bruyne, alifanikiwa kushinda mataji matatu ya kihistoria msimu uliopita huku klabu yake ya Manchester City ikipata ushindi wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa pamoja na mataji mengine mawili ya nyumbani.
De Bruyne, ambaye pia ametangazwa nahodha mpya wa Ubelgiji, alimaliza kampeni ya msimu wa Ligi ya Premia kwa kutoa pasi nyingi zaidi (16) kwa mara ya tatu. Pia alifunga mabao mengi (saba) kuliko mchezaji mwingine yeyote kwenye Ligi ya Mabingwa 2022/23 na kunyakua tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi katika mechi nne kati ya mechi kumi zake alizocheza.
Mshambulizi aliyevunja rekodi ya Manchester City Erling Haaland ni mmoja wa wachezaji watatu walioteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Kiume wa UEFA 2022/23.
Magoli, magoli na magoli zaidi, Haachi kufunga! Katika msimu wake wa kwanza akiwa City, Haaland alionekana kuwa na uraibu wa kufunga, akiwa na mabao 12 ya kuvutia kwenye Ligi ya Mabingwa ya UEFA - manne zaidi ya mpinzani wake wa karibu, Mohamed Salah wa Liverpool - na kuvunja rekodi ya 36 kwenye Premier League.
Nyota huyo wa Norway pia alikuwa mchezaji mwenye umri mdogo na wa kufikisha mabao 35 kwa jumla ya Ligi ya Mabingwa kwa wepesi, na alitwaa medali yake ya kwanza ya ushindi kwenye dimba hilo na kuambatana na zile alizonyakua City ikishinda Ligi Kuu na Kombe la FA.
Haaland ameingia kwenye vitabu vya historia kwa kuwa nyota wa tatu kufunga mabao matano katika mechi moja ya Ligi ya Mabingwa baada ya Lionel Messi na Luiz Adriano.
Wakati huo huo, wawaniaji wa tuzo za Kocha Bora wa mwaka kutoka UEFA, 2023 wametangazwa huku Josep Guardiola, Simone Inzaghi, Luciano Spalletti waniwania tuzo hiyo kufuatia uongozi wao bora kwa timu zao.
Kwa upande wa wanawake, Kocha wa England, Sarina Wiegman ambaye aliiongoza timu hiyo kutinga fainali yake kwanza ya Kombe la Dunia la Wanawake, atawania tuzo hiyo dhid ya na Jorge Vilda, ambaye aliisaidia timu yake ya Uhispania kushinda Kombe la Dunia la wanawake, na Jonatan Giraldez wa Barcelona ambao wameteuliwa kuwania kocha bora wa mwaka wa UEFA wa Wanawake 2022/23.
Kwa upande wa soka ya wanawake, Aitana Bonmatí, Olga Carmona, na Sam Kerr wameteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Kike wa UEFA 2022/23.
Mshambulizi wa Australia na Chelsea, Sam Kerr atawania tuzo hiyo na wahispania walioteuliwa, Aitana Bonmati na Olga Carmona.