Msumbiji waikaba koo Misri kwa sare ya 2-2 katika mechi - AFCON

Msumbiji waikaba koo Misri kwa sare ya 2-2 katika mechi - AFCON

asdf
Misri itacheza dhidi ya Ghana Januari 18, 2024 katika mechi ya pili ya Kundi B. / Picha: AFP

Misri na Msumbiji zilitoka sare ya 2-2 katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi B katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 Jumapili.

Mostafa Mohamed alikuwa ameifungia Misri bao la kwanza dakika ya pili, lakini Msumbiji aliyechangamka walisawazisha dakika ya 55 kupitia kwa Witiness Chimoio almaarufu Witi.

Clesio Bauque kisha akaiweka Msumbiji mbele katika dakika ya 58.

Misri ilipambana, na kuishinikiza Msumbiji katika juhudi za kupata bao la kusawazisha.

Katika dakika ya saba ya muda wa nyongeza wa kipindi cha pili, Mohamed Salah alifunga mkwaju wa penalti na kuwavuta Misri.

Mtihani wa Ghana

Misri na Msumbiji sasa wana pointi moja. Timu nyingine mbili za Kundi B - Ghana na Cape Verde - zitacheza baadaye Jumapili.

Mechi inayofuata ya Misri itakuwa dhidi ya Ghana siku ya Alhamisi na baadaye dhidi ya Cape Verde Jumatatu, Januari 22.

Msumbiji, kwa upande mwingine, itacheza dhidi ya Cape Verde siku ya Alhamisi na dhidi ya Ghana Januari 22.

TRT Afrika