Mpiganaji wa Cameroon Mixed Martial Arts, Francis Ngannou ametia saini mkataba mpya wa ushirikiano na Ligi ya Professional Fighters baada ya kutengana na kampuni ya kukuza mapambano ya UFC.
Ngannou alijiondoa katika mkataba wake wa UFC Desemba mwaka jana baada ya kusema madai yake ya bima ya afya na ufadhili wa kibinafsi yamekataliwa.
Katika taarifa ya video kwenye ukurasa wake wa YouTube, Ngannou alisema "Ulikuwa mchakato mrefu na wa kufikiria sana na huu ndio uamuzi bora ninaofanya sio kwa ajili yangu tu bali kwa familia yangu."
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 atapigania PFL pekee katika kitengo chake cha mpambano wa kulipia unapotaza. Ngannou, ambaye alimshinda Stipe Miocic mnamo 2021 na kushinda taji la UFC, pia atakuwa mwenyekiti na mmiliki sawa wa PFL Afrika.
Mnamo Januari, rais wa UFC Dana White alimvua Ngannou mkanda wake wa UFC Heavy Weight baada ya kutengana. Ngannou ana rekodi mchanganyiko za karate ametwaa ushindi mara 17, na kupoteza mara 3 huku michuano 12 katia ya 17 aliyoshinda ilikua ni kwa 'knockout'