Michuano ya kufuzu kombe la mataifa bora Ulaya itaendelea jumapili huku mataifa mbalimbali yakilenga kutua UEFA EURO 2024 kwa kujizolea pointi muhimu katika mechi za kufuzu kupitia makundi.
Mataifa ya Italia, Hungary na Denmark yamekaribia kufuzu kwa dimba la mataifa bora ulaya EURO 2024 baada ya kuandikisha ushindi siku ya jumamosi kwenye mechi za 7 raundi ya kufuzu michuano hiyo.
Uturuki itakuwa nyumbani dhidi ya Latvia baada ya kuifanya Croatia kupoteza mechi yake ya kwanza katika michuano 11 ya kufuzu kwa EURO kwa kuwapiga 1-0.
Barış Alper Yılmaz alikuwa shujaa wa Uturuki kwani ushindi huo pia uliiwezesha Uturuki kuipiku Croatia kwenye jedwali la kundi D baada ya ushindi mgumu huko ugenini Osijek.
Kocha mpya wa Uturuki Vincenzo Montella alianza mapema kazini kwa kuanza na kushinda kwa muda wake na Uturuki, ambao waliwatesa wenyeji wao kwa kuwapa pigo lao la kwanza nyumbani katika mechi za kufuzu kwa EURO.
Mbali na hayo, mchuano wa wiki hii unaoonekana kuvutia zaidi katika mechi 8 ni kati ya England na Italia watakaokabiliana ugani Wembley.
England inalenga kufuzu kwa fainali yake ya tisa kati ya mashindano 10 ya kombe la EURO.
Hata hivyo, Italia itakuwa inalenga kulipiza kisasi dhidi ya England baada ya kupoteza nyumbani Naples 2-1.
Ratiba ya siku ya Jumapili 15 Oktoba 2023
Mechi za Kundi A: Georgia vs Cyprus, Norway vs Uhispania
Mechi za Kundi D: Uturuki vs Latvia, Wales vs Croatia
Mechi za Kundi E: Czech vs Visiwa vya Faroe, Poland vs Moldova
Mechi za Kundi I: Uswizi dhidi vs Belarus, Romania vs Andorra