Mama Samia Suluhu Hassan amewapongeza Wanasimba wakiwemo wachezaji , wasimamizi wa klabu na mashabiki kwa kujitolea katika kuhudumia jamii ambapo walijitolea katika shughuli za kuhudumia jamii.
''Nimefahamishwa na kujionea mwenyewe mambo kadhaa ya kutia moyo sana.''Amesema Rais Samia. ''Mambo haya nipamoja na wanasimba kusambaza upendo kwa makundi mbali mbali ikiwemo ya kina mama, watoto yatima, kutoa vifaa vya kufanyia usafi katikamikoa tofauti na kuchangia damu salama kwa ajili ya wahitaji.'' Aliongeza Mh Samia.
Rais Samia pia aliwapongeza Wanasimba kwa kuutangaza utalii wa Tanzania 'walipopeleka kibegi' katika kilele cha mlima Kilimanjaro. ''Kibegi hicho kwa kweli kimeitangaza Tanzania.'' Amesema Rais Samia.
Rais Samia alipokea Jezi mpya iliyochapishwa jina lake mgongoni.
Simba SC ilizindua Jezi yake mpya kileleni mwa mlima KIlimajaro, na kuwavutia wengi.
Jezi za kwanza za timu hiyo zilizinduliwa zikiwa na majina ya viongozi wa Tanzania wakiongozwa na Mama Samia Suluhu Hassan, Kassim Majaliwa, Husssein Mwinyi, Philip Mpango, Rais wa heshima wa Simba Mohammed Dewji, na Spika wa bunge Tulia Ackson.
Simba imeeleeza kuwa jezi zenye majina ya viongozi hao zitapigwa mnada na pesa hizo kutumika kwenye ujenzi wa wodi ya afya za kina mama katika vituo vya afya vikiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Zanzibar. Aidha, imeahidi kutoa zawadi kwa wahusika walioshiriki katika uzinduzi wa jezi hiyo mlima Kilimanjaro.
Simba imejiimarisha kwa kuwasajili wachezaji saba wapya ambapo walikaribishwa kwa safari ya uturuki walikopiga mechi 3 za kirafiki na kukaa kambini kupata msasa.
Simba SC imeandaa mechi na Power Dynamo wa Zambia kama kilele cha maadhimisho ya siku ya SImba. Hii ikiwa mara ya pili kwa klabu hizi mbili kukutana.
Simba ilipiga kambi ya wiki tatu nchini Uturuki kama njia ya kujizoeza kwa wachezaji wapywa waliosajiliwa na kujiandaa kwa msimu mpya.
Uwanja wa Benjamin Mkapa, Temeke ulifurika mashabiki 60,000 ambao wanasemekana walinunua tikizi zote siku mbili kabla ya siku ya dhifa.
''Mambo kama haya yanaonyesha namna gani michezo inaweza kuleta amani na utulivu na kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii,'' amesema Rais Samia alipohutubia hadhira katika uwanja huo.
''Ahadi yangu ya kununua magoli iko palepale. Timu za Tanzania zikacheze zituletee ushindi.'' Alitangaza mama Samia.