Uhispani ndiye mabingwa wa Dunia Kombe la Dunia la Wanawake 2023 liilochezwa NewZealand na Autralia / Picha X FIFA WWCUP

Kwanza kabisa, kofia inavuliwa kwa ajili ya heshima ya nahodha Olga Carmona ambaye aliibuka kama shujaa nakuweka historia katika timu ya La Roja kwa bao zuri zaidi lililofanikisha timu hiyo kunyakua taji kuu la kwanza na kukamilisha usafishaji wa kipekee wa mataji ya FIFA katika U-17, U-20 na kiwango cha juu.

Olga Cramona

Olga anayechezea klabu ya Real Madrid kama beki wa kushoto alitikisa wavu wa England dakika ya 29, ambalo ndilo bao la ushindi na bao la pekee katika mechi hiyo.

Tuzo la mchezaji mwenye umri mdogo lilimuendea Salma Paralluelo / Picha X -FIFA WWORLD CUP

Tuzo la mchezaji mwenye umri mdogo lilimuendea Salma Paralluelo. Majina yake kamili ni Salma Celeste Paraluelo Ayingono na mwanasoka wa kulipwa wa Uhispania na mwanariadha wa zamani ambaye anacheza kama mshambliaji wa kushoto katika klabu ya Liga F FC Barcelona. Salma ana miaka 19.

Mary Earps, Kipa wa England ndiye msindi wa tuzo la Golden Glove katika FIFA Kombe la Dunia la Wanawake 2023 /Picha : X Mary Earps

Tuzo la Golden Glove lilimuendea Mary Ear wa England. Mary Alexandra Earps ni mchezaji wa kulipwa kutoka England ambaye anacheza kama golikipa wa Manchester United katika Ligi Kuu ya Wanawake na timu ya taifa ya England, alishikilia nafasi ya naibu wa nahodha wa kikosi cha England katika michuano ya FIFA Kombela Dunia. Ana miaka 30.

Hinata Miyazawa ndiye mshindi wa tuzo la Golden Boot katika FIFA Kombe la Dunia la wanawake 2023 Picha : X FIFA WWCUP 

Hinata Miyazawa ni mwanasoka wa kulipwa wa Japani ambaye anacheza kama kiungo wa klabu ya WE League Mynavi Sendai na timu ya taifa ya wanawake ya Japan. Japan waliacha mtikisiko katika shindano hili kwani walifika robo fainali ambapo waliondolewa na Sweden 2-1.

Aitana Bonmati ndiye bingwa wa tuzo la Golden Ball katika KOmbe la Dunia la Wanawake 2023 / Picha X FIFA WWCUP

Aitana Bonmatí Conca ni mchezaji wa kulipwa wa Uhispania ambaye anacheza kama kiungo wa klabu ya Liga F Barcelona na timu ya taifa ya wanawake ya Uhispania. Bonmatí amekuwa na Barcelona tangu 2012, akikua kupitia La Masia kwa miaka sita.

TRT Afrika