Timu ya taifa ya voliboli ya wanawake ya Kenya, Malkia Strikers, imeanza safari yake ya kuzoa taji lake la 10 la barani Afrika vyema, baada ya kujipa ushindi mnene wa 3-0 dhidi ya Rwanda kwenye mechi ya ufunguzi ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya Voliboli kwa Wanawake, Yaoundé, Cameroon.
Kenya, mshindi wa taji hilo mwaka 2015, imefika fainali mara tatu kwenye makala yaliyopita huku ikipokea ushindani mkali kutoka Cameroon.
Malkia Strikers, imeanza mechi yake ya Kundi 'B' kwa kuitesa Rwanda kwa seti tatu za 3-0 za (25-16, 25-20, 25-17) huku ikiwa kundi moja na Morocco, Rwanda, Uganda, Burkina Faso, na Lesotho.
Kwenye mechi za awali, Morocco iliicharaza Burkina Faso 3-0 huku Nigeria ikiilaza Mali 3-0.
Wakati huohuo, wenyeji na mabingwa watetezi Cameroon wako katika kundi 'A', pamoja na DR Congo, Nigeria, Algeria, Burundi, Mali na Misri. Makala ya 21 ya Mashindano ya voliboli kwa wanawake 2023 imeandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Wavu barani Afrika (CAVB) huku michuano hiyo ikitumika kufuzu kwa Mashindano ya Dunia yajayo