Bruno Fernandes na Casemeiro wafunga mabao mawili dhidi ya Leicester City, huku Garnacho akijinyakulia bao moja. /Picha: Manchester United

Ruud Van Nistelrooy, aliyekuwa mshambuliaji maarufu wa Manchester United na sasa kocha wa muda, amerudisha furaha na matumaini kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kuiongoza kwa kishindo na ushindi mkubwa wa mabao 5-2 dhidi ya Leicester City kwenye Uwanja wa Old Trafford, katika michuano ya Kombe la Carabao.

Ruud Van Nistelrooy kocha wa muda wa Manchester United, amewahi kuchezea timu hiyo toka 2001 hadi 2006. /Picha: Manchester United

Manchester United ilikuwa kwenye hali ya kuyumba chini ya kocha Erik ten Hag, ambaye hatimaye alitimuliwa.

Lakini sasa, upepo unaonekana kubadilika!

United itavaana na Tottenham Hotspur kwenye robo fainali, baada ya Tottenham kuichapa Manchester City mabao 2-1.

Nayo Arsenal itapambana na Crystal Palace, Liverpool dhidi ya Southampton, huku Newcastle United ikiingia vitani na Brentford.

TRT Afrika