Galatasaray iliitundika Molde 3-2 baada ya Fredrik Midtsjo kufunga bao la kunyakua ushindi katika kipute cha mkondo wa kwanza wa mechi za mchujo kufuzu kwa UEFA Champions League.
Molde ilifunga bao la kuongoza wakati Martin Ellingsen alipopachika kutumia kicha chake kunako dakika ya nane kwenye Uwanja wa Molde Stadion.
Sergio Oliveira aliisawazishia timu yake 1-1 kwa kufunga mkwaju wa ikabu dakika ya 25.
Baada ya dakika nne, Mauro Icardi alipiga shuti safi kupitia mguu wa kulia katika eneo la hatari baada ya Yunus Akgun pasi ya mbali ya darasa.
Baadaye dakika ya 44, Yunus Akgun aliifungia Galatasaray lakini bao lake lilikataliwa baada ya mtambo wa VAR kuamua kuwa Dries Mertens alimchezea vibaya mchezaji wa Molde.
Beki wa Molde, Kristoffer Haugen alimaliza kwa mwendo wa kasi na kusawazisha bao kwa 2-2 katika dakika ya 56.
Nguvu mpya, kiungo wa kati wa Norway Midtsjo, aliinuka kutoka benchi dakika ya 82 na kutoa goli katika dakika ya 93. Icardi alimpoteza mlinzi wake na kutoa pasi kwa Midstjo ili kufunga bao rahisi la wazi.
Pande hizo zinajiandaa kwa Mchezo wa mkondo wa pili utakaofanyika katika uwanja wa nyumbani wa Galatasaray, Ali Sami Yen Sports Complex mnamo Agosti 29.