#KOK69 : Football: Women's World Cup - 1st round day 2 / Photo: AFP

Katika viwango vya hivi punde vilivyochapisha na FIFA, ikiwa na mabadiliko kadhaa chanya kwa Afrika, Nigeria imesalia kuwa taifa bora zaidi Afrika huku Super Falcons wakiwa wamepanda nafasi nane na kiwa tu nje kidogo ya timu 30 bora (32),

Licha ya kushiriki Kombe la Dunia la Wanawake, kwa mara yao Morocco, wamesonga nafasi 14 juu kwa kufanya mruko mkubwa zaidi kutoka 78 hadi 58.

Timu ya pili kuchupa kwa ukubwa katika viwango hivyo ni Afrika Kusini ambapo miamba wa Banyana Banyana ilisonga mbele kwa nafasi 9 na kushika nafasi ya 45 kwenye msimamo.

Copper Queens ya Zambia pia walifanya maendeleo mazuri katika viwango vyao baada ya kutoka nafasi ya 77 hadi ya 69.

TRT Afrika