Faith Kipyegon kuwania tuzo ya mwanariadha bora wa kike duniani 2023

Faith Kipyegon kuwania tuzo ya mwanariadha bora wa kike duniani 2023

Orodha ya wawaniaji 11 wa tuzo ya wanariadha bora wa kike duniani 2023 imetolewa
Kipyegon ni miongoni mwa wawaniaji 11 wa tuzo ya wanariadha bora wa kike duniani 2023. / Picha: AFP

Wanariadha hao walichaguliwa na jopo la kimataifa la wataalam wa riadha, linalojumuisha wawakilishi kutoka maeneo yote sita ya bara ya riadha ulimwenguni.

Mchakato wa upigaji kura kwa wanariadha bora wa dunia wa mwaka wa 2023 umefunguliwa wiki hii kabla ya tuzo za riadha duniani 2023.

Tigist Assefa, Ethiopia, Mbio za Marathon

  • Mshindi wa mbio za marathon za Berlin
  • Rekodi ya dunia ya marathon

Femke Bol, Uholanzi, 400m/400m kuruka Vihunzi

  • Bingwa wa dunia mbio za 400m kuruka vihunzi
  • Ameweka rekodi ya dunia ya ndani ya mita 400

Shericka Jackson, Jamaika, 100m/200m

  • Bingwa wa dunia wa mita 200 na mshindi wa medali ya fedha ya mita 100
  • Bingwa wa mbio za ligi ya Diamond 100m na 200m

Faith Kipyegon, KEN, 1500m/mile/5000m

  • Mshindi wa mbio za 1500m and 5000m duniani
  • Ameweka rekodi mpya katika mbio za 1500m, maili na 5000m

Kenya Faith Kipyegon

Haruka Kitaguchi, Japani, mrushaji mkuki

  • Bingwa wa dunia
  • Bingwa wa ligi ya Diamond

Yaroslava Mahuchikh, Ukraine, mruka juu

  • Bingwa wa dunia
  • Bingwa wa ligi ya Diamond

Maria Perez, Uhispania, mbio kutembea

  • Bingwa wa dunia 20km na 35km mbio za kutembea
  • Anashikilia rekodi ya dunia katika 35km mbio kutembea

Gudaf Tsegay, Ethiopia, 5000m/10,000 m

  • Mshindi wa dunia wa mita 10,000
  • Mshindi wa ligi ya Diamond mbio za 5000m na ameweka rekodi ya dunia

Sha'carri Richardson, 100m/200m

  • Bingwa wa dunia katika mbio za mita 100
  • Mshindi wa medali ya shaba duniani katika mbio za mita 200

Sha'Carri Richardson

Yulimar Rojas, Venezuela kuruka mara tatu

  • Bingwa wa dunia
  • Bingwa wa ligi ya Diamond

Winfed Yavi, Bahrain, 3000m kuruka vihunzi na maji

  • Mshindi wa Dunia
  • Bingwa wa ligi ya Diamond na muda unaoongoza duniani

Shughuli ya upigaji kura kumchagua mwanariadha bora wa dunia wa mwaka itafungwa saa sita usiku, ifikapo Jumamosi Oktoba 28.

Mchakato huo wa kupiga kura utafuatwa na tangazo la wanawake watano na wanaume watano bora wa mwisho litakalofanywa shirikisho la riadha dunini tarehe 13-14 Novemba.

Washindi wa mwanariadha bora wa kike na wa kiume watatangzwa rasmi kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii ya shirikisho la riadha duniani World Athletics tarehe 11 Desemba.

TRT Afrika