Mmiliki wa rekodi za mbio za mita 5000, ametambulika kwa kuteuliwa kwa mara nyingine kuwania tuzo ya wanaspoti bora duniani, maarufu LAUREUS kwa kuwa mwanamke wa kwanza kukimbia kwa kasi zaidi kuwahi kutokea katika mita 5000 kwenye historia.
Kipyegon, kutoka Nakuru, maeneo ya Bonde Ufa nchini Kenya alianza safari yake ya raisha kimataifa katika mashindano ya dunia ya riadha huko Bydgoszcz mnamo 2010.
Disemba mwaka jana, Kipyegon alitunukiwa mwanariadha bora wa kike Duniani baada ya kuwa na msimu wa ajabu na mafanikio.
Kipyegon, ndiye bingwa wa Mita 1,500 katika Olimpiki 2016 na 2021.
Mwanasoka Aitana Bonmatí (Uhispania), mshindi wa Kombe la Dunia kwa wanawake, Ligi ya Mabingwa na Liga F pamoja na Ballon D'or Féminin.
Mwanariadha Sha'carri Richardson (Marekani) mshindi wa dhahabu katika mita 100 na mbio za 4 x 100 mita relay.
Mwanariadha Shericka Jackson (Jamaica) mshindi wa dhahabu mita 200 katika mashindano ya Dunia.
Mikaela Shiffrin (Marekani) kuteleza kwenye barafu Alpine ambaye ni kiongozi wa wakati wote katika Ushindi wa Kombe la Dunia.
Mchezaji wa tenisi Iga Świątek (Poland), ambaye ni mshindi mara tatu wa michuano ya Ufaransa (French Open) na kupata tena nafasi bora Duniani, fainali za WTA.