Fainali ya Ligi ya Mabingwa ya UEFA 2023/24 itafanyika kwenye Uwanja wa Wembley, London Jumamosi 1 Juni. / Picha: AP

Droo ya hatua ya makundi kuwania ubingwa wa soka Ulaya, UEFA Champions League 2023/24 itafanyika leo Alhamisi kwenye Jukwaa la Grimaldi huko Monaco, baada ya miaka mitatu ugenini.

Arsenal, iliyomaliza nafasi ya pili msimu wa 2005/2006, imerejea kucheza Champions League katika michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2016/17.

Manchester United, ambao iliyotwaa taji la Ligi ya Mabingwa mara tatu, pia wanarejea kwenye michuano hiyo, baada ya kumenyana kwenye Ligi ya Europa msimu uliopita.

Newcastle United, wameingia kwa mara ya kwanza katika hatua ya makundi ya michuano hiyo tangu msimu wa 2002/03.

Droo hiyo itashirikisha jumla ya timu 32 zikiwemo timu 26 zilizofuzu moja kwa moja pamoja na timu sita zilizofuzu kupitia mtoano na kwa kushinda mechi zao za mchujo.

Fainali ya Ligi ya Mabingwa ya UEFA 2023/24 itafanyika kwenye Uwanja wa Wembley, London Jumamosi 1 Juni.

Orodha ya timu zilizothibitishwa kushiriki mechi za hatua ya makundi zikiwania ligi ya Mabingwa 2023/24.

  • UINGEREZA: Arsenal, Manchester City, Manchester United, Newcastle
  • UHISPANIA: Atlético, Barcelona, Real Madrid, Real Sociedad, Sevilla
  • ITALIA: Inter, Lazio, Milan, Napoli
  • UJERUMANI: Bayern, Dortmund, Leipzig, Union Berlin
  • UFARANSA: Lens, Paris
  • URENO: Benfica, Braga, Porto
  • UHOLANZI: Feyenoord, PSV
  • AUSTRIA: Salzburg
  • SCOTLAND: Celtic
  • SERBIA: Crvena zvezda
  • UKRAINE: Shakhtar Donetsk
  • BELGIUM: Antwerp
  • USWIZI: Young Boys
  • DENMARK: Copenhagen
  • UTURUKI: Galatasaray

Msimu huu ndio utakuwa wa mwisho wa muundo wa timu 32 kwani shindano la msimu ujao litapanuka hadi timu 36.

TRT Afrika