Nahodha wa Ureno na AL Nassr Cristiano Ronaldo anatarajiwa kushiriki mapigano ya miereka maarufu ‘WWE Crown Jewel’ nchini Saudi arabia.
Bila shaka, Ronaldo atashiriki kwenye mapigano hayo kwa kulipwa mkwanja ili kujipima nguvu nje ya soka.
Wamiliki wa mapigano ya mieleka ya Dunia WWE wanadaiwa kupanga kumshirikisha Cristiano Ronaldo kwenye onyesho lijalo la WWE Crown Jewel.
Pigano la ‘Crown Jewel’ la mwaka huu litafanyika Novemba 4 wakati WWE itakaporejea Saudi arabia kwa mara ya pili baada ya shindano la mwezi Mei, ambapo jiji la Jeddah lilikuwa mwenyeji wa makala ya 2023 ya pigano maarufu la usiku wa Mabingwa.
WWE iliwahi kuandaa mapigano manne ya awali ya ‘Crown Jewel’ nchini Saudi Arabia tangu 2018, na pia maonyesho mengine kadhaa.
Mnamo Aprili mwaka huu, wamiliki wa mapigano maarufu duniani UFC walinunua WWE ambao huku wakionekana kuwa na hamu ya kuongeza umaarufu wa Crown Jewel na kuimarisha mapato yao kwa kuwa na Ronaldo kwenye mashindano hayo.
Hili linaonekana kama fursa kwa Ronaldo, mwenye umri wa miaka 38, huku akiendelea kuonyesha utulivu wake kwenye klabu ya Al Nassr ya ligi kuu ya Saudia, Saudi Pro League.
Mnamo Desemba 2022, Mreno huyo alisaini mkataba wa miaka miwili na nusu wenye thamani ya dola milioni $215 kwa msimu.