Kiungo na mshambuliaji wa Chelsea, Cole Palmer, alifunga mabao manne na kuiweka Chelsea karibu ya timu sita bora kwenye jedwali ya Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League) baada ya ushindi wa 6-0 dhidi ya Everton siku ya Jumatatu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekuwa nyota ya kun'gaa kwa timu yake, ingawa timu yake kutofanya vizuri kataka ligi, ana mabao 20 sawa na mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland, wakiwa kwenye mchakato wa kuwania Kiatu cha Dhahabu (Golden Boot).
Palmer alipatia ushindi timu yake, huku akifunga mabao matatu ndani ya dakika 30 kabla ya Nicolas Jackson pia kufunga kabla ya kipindi cha mapumziko.
Hata hivyo, usiku huo haukupita bila misukosuko kwa Chelsea, kwani Palmer alilazimika kuwazuia wachezaji wenzake Jackson na Noni Madueke kufunga bao la nne kwa mkwaju wa penalti. Akifunga hilo bao la nne mwenyewe.
"Hatuwezi kuwa na tabia kama hii. Niliwaambia hii ni mara ya mwisho nitaruhusu haya kutokea," alisema Pochettino baada ya ushindi wake mkubwa zaidi akiwa kocha wa Chelsea hadi sasa.
Nafasi ya tisa
Licha ya msururu wa mechi nane bila kufungwa katika ligi, Chelsea wanasalia katika nafasi ya tisa lakini sasa wapo nyuma ya Newcastle kwa pointi tatu tu, huku wakiwa na mchezo moja zaidi.
Aidha watamenyana na Manchester City kwenye nusu-fainali ya Kombe la FA siku ya Jumamosi, wakiwa na imani kwamba wanaweza kumaliza tamaa za mabingwa hao za kusaka mataji matatu kwa mara mbili mfululizo.
"Jambo muhimu zaidi kwa sasa ni kujenga timu ambayo ni thabiti," aliongeza Pochettino.
"Hatukuwa thabiti vya kutosha. Tunahitaji kujifunza na kujifunza haraka."
Kuvunjika moyo kwa Everton
Kucharazwa kwa mabao sita, kuliwavunja moyo Everton, ikiwa bado iko kwenye hatari ya pointi mbili tu ya kushushwa daraja.
Siku ya Jumapili, Nottingham Forest watatembelea Goodison Park wakiwa na pointi moja tu nyuma ya Everton, wao pia wakiwa hatari ya kuteremka daraja ya ligi ya chini, huku timu ya Sean Dyche watahitaji kuimarika katika ncha zote mbili za uwanja ili kurefusha uwepo wao wa miaka 70 kwenye ligi kuu.
"Nimejiskia aibu kama mtu binafsi, na kama mmoja katika sehemu ya timu, katika wakati wangu wote mpirani," alisema beki wa Everton, James Tarkow.
Everton ilipata pigo kabla ya mechi kuanza kwa kumkosa mshambulizi Dominic Calvert-Lewin kutokana na jeraha la misuli ya paja.
Naibu wake Beto alipoteza nafasi nzuri ya kufunga bao aliposhindwa kufunga kwa njia ya krosi ya Seamus Coleman.
Palmer kwa upande wake hakupoteza fursa ya kung'aa na kujitosa kwenye kinyanganyiro cha kuwania kutawazwa kama mchezaji bora wa mwaka wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Bila shaka Manchester City lazima watakua wanajuta kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kuondoka kwa bei ya dola milioni 50 tu.