Postecoglou aishtumu VAR Baada ya Chelsea kuipa spurs kichapo cha kwanza Premier League msimu huu

Postecoglou aishtumu VAR Baada ya Chelsea kuipa spurs kichapo cha kwanza Premier League msimu huu

Tottenham ilinyimwa mabao mawili na VAR huku Cristian Romero na Destiny Udogie wakila kadi nyekundu katika mechi ya ajabu ya Ligi kuu.
Postecoglou alidai kwamba angependelea mwamuzi na manaibu wake kuwa na uamuzi wa mwisho juu ya maamuzi muhimu, badala ya afisa wa VAR ambaye hata hayuko kwenye uwanja. / Picha: AFP

Kocha wa Tottenham Ange Postecoglou alikiri kwamba hapendi VAR wakati alipolaumu ushawishi wa mfumo huo wa kutathmini matukio mechini, kwenye ushindi wa "nje ya udhibiti" wa 4-1 dhidi ya Chelsea Jumatatu.

Imekuwa ni mara ya kwanza Tottenham kufungwa tangu Postecoglou alipochukua jukumu la kuinoa timu hiyo msimu huu huku ikiwanyima nafasi ya kupaa juu katika Ligi Kuu EPL.

Kuondolewa mechini kwa Romero, kwa kumchezea visivyo Enzo Fernandez, na Udogie, ambaye alipata kadi ya pili ya njano kwa kumuumiza Raheem Sterling, ulionekana sahihi kufuatia ukaguzi zaidi, kama pamoja na kukataliwa kwa magoli ya Son Heung-min na Eric Dier.

Mshambulizi wa Chelsea Nicolas Jackson alifunga hat triki katika kipindi cha lala salama na kufunga kazi debi ya London kwa kuipa Chelsea ushindi baada ya Cole Palmer kusawazisha goli la ufunguzi la mapema la Dejan Kulusevski wa Tottenham.

Hata ingawa VAR ilikataa mabao matatu yaliyofungwa na Chelsea, Postecoglou aliachwa na hasira kwa muda uliotumika kusubiri maamuzi yafanyike.

"Nilihisi kama nilikuwa nimesimama nikingojea mambo yatokee kwa kuingilia kati kwa VAR", alisema.

"Kutakuwa na ukaguzi wa kina wa kila uamuzi huko nje, na nadhani kwamba ndio njia mchezo unavyoeleka na mimi sipendi mambo kama hayo.

Postecoglou alidai kwamba angependelea muamuzi na manaibu wake kuwa na uamuzi wa mwisho juu ya maamuzi muhimu, badala ya afisa wa VAR ambaye hata hayuko uwanjani.

AFP