Bondia Carl Jammes "Wonderboy" Martin wa Philipinnee na Oscar Duge wa Tanzania. Picha: Carl Jammes "Wonderboy" Martin

Bondia wa Tanzania Oscar Duge wa Tanzania amepoteza pambano la uzani wa super bantam dhidi ya Carl Jammes "Wonderboy" Martin wa Philippines.

Carl Jammes "Wonder Boy" amepata ushindi huo dhidi ya Oscar Duge kupitia Uamuzi wa pamoja kwenye pigano la raundi 10 na kusalia na rekodi ya kutoshindwa baada ya kuibuka kwa pointi (99-91 / 98-92 / 99-91).

'Wonderboy', mwenye umri wa miaka 24, anaorodheshwa katika nafasi ya 4 na shirikisho la ndondi IBF na nambari 9 katika WBO kama uzito wa juu zaidi. Yeye ndiye bingwa wa sasa wa IBF Pan-Pacific na aliwahi kushikilia mikanda ya WBA Asia na WBO Oriental Youth.

Kwa sasa Martin, amesalia kwenye nafasi ya 4 katika IBF na nambari 9 katika WBO kama uzito wa juu zaidi. Yeye ndiye bingwa wa sasa wa IBF Pan Pacific na aliwahi kushikilia mikanda ya WBA Asia na WBO Oriental Youth.

"Ninahisi changamoto ni kufuta rekodi yake. Lengo langu, ni kuwa bondia wa kwanza kuvunja rekodi yake ya kutopoteza kwa mtoano. Hilo litakuwa ," alisema Martin wakati wa upimaji uzito rasmi katika ukumbi wa mazoezi wa Elorde huko Manila.

Hata hivyo, Duge mwenye umri wa miaka 26, akiwa na uzito wa pauni 118.4, amedumisha rekodi yake ya kutopoteza kupitia knock-out na kuendeleza umahiri wake huku akiwa na rekodi ya matokeo ya 11-5-2.

Licha ya kuwa pambano hilo la uzani wa super bantam halikuwa ni la taji rasmi, Oscar alikuwa akilenga kuondoa fomu bora ya Martin ulimwenguni. ''Hii ni nafasi yangu kuleta sifa kwa familia yangu na kwa ajili ya Tanzania,” alisema Duge kwenye mahojiano kabla ya kuingia ulingoni.

TRT Afrika