Mashindano ya Chess ya Vijana ya Kiafrika yanatumika kama hatua ya kufuzu kwa Mashindano ya Dunia ya Chess. Picha: TRT Afrika

na

Takunda Mandura

Katika onyesho la filamu ya kuvutia kutoka katika filamu ya wasifu iliyoongozwa na Mira Nair ya Mwaka 2016, ijulikanayo kama Queen of Katwe, mwigizaji anayecheza mchezo wa Chess wa Uganda anayeitwa Phiona Mutesi mwenye umri wa miaka 10 akiwa na mshauri wake Robert Katende kila mmoja akiwa mshindani wa mwenzake kila mtu anatulia kwa sehemu yake kila sekunde kabla ya kukata shauri na kuanza kwa shindano hilo ambapo Katende anamkemea kwa upole, "Hapana...hapana, Phiona. Usimdokeze mfalme wako haraka hivyo." akimaanisha usimzidi mtu Aliyekuzidi kiasi hicho.

Mbali na burudani ya Hollywood ya maisha yenye hadhi ya peke yake unaweza kusema hadhi ya kifahari au ardhi ya kibingwa, ipo pia Chivhu nchini Zimbabwe, Grace Zvarebwa mwenye umri wa miaka 12 amekuwa akifanya mazoezi kwa miaka minne ya sanaa.

Wakati huo huo, msichana huyu mnyenyekevu aliyezaliwa katika familia ya wakulima wadogo wadogo kutoka mji ulioko kilomita 146 kusini mwa mji mkuu wa Harare ameandika jina lake kama mtu maarufu anayetarajiwa duniani kwa kuwa bingwa wa taifa wa Zimbabwe wa mchezo wa chess yani Sataranji au (Bao)kwa kiswahili cha Pwani ya Bahari ya Hindi.

Grace anatamani kuwa FIDE Grandmaster, sio kidogo, na kuwashauri wengine kama yeye nyumbani nchini Zimbabwe ili wawe mabingwa katika mchezo huo.

"Mnamo Juni, nilishinda katika mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 16 nchini Zimbabwe, na tunatakiwa kusafiri hadi Misri wiki ijayo kwa ajili ya michuano ya Afrika kwa Vijana ya Sataranji. Natarajia ufadhili ili niweze kwenda huko na kushinda mashindano hayo," Grace amewaeleza TRT Afrika. "Nitatumia zawadi ya pesa kusaidia wazazi wangu na kusaidia wenzangu na kufadhili wenzangu pale itakapobidi."

Vijana wa Zimbabwe wana ndoto ya kufanikiwa nje ya nchi. Picha: TRT Afrika

Tangu aanze mchezo huo miaka minne iliyopita, Grace ameshinda zaidi ya medali 15 katika mashindano yote Zimbabwe. Katika baadhi ya hayo, aliwashinda wachezaji karibu mara mbili ya umri wake. Ndoto yake ya kufanikiwa nje ya nchi yake na kwa sasa yametokea mashindano yanayowashirikisha na wengine wengi kama yeye, kutokana na mipango ya ushauri kama ile iliyomtoa Phiona Mutesi kutoka kwa umaskini na kumfanya kuwa maarufu. Malkia wa Chivhu

Godknows Dembure, ambaye anafundisha katika Shule ya Msingi ya Makumimavi, ambayo ni sehemu ya kazi zake huko Chivhu sehemu ambapo Katende alifanya kazi huko Katwe, kitongoji duni katika mji mkuu wa Uganda wa Kampala, baada ya kukutana na Phiona aliyeacha shule wakati wa mahubiri yanayoendeshwa na wamisionari.

Katika Shule ya Msingi ya Nharira, mahali alipofanya kazi hapo awali, Dembure alianzisha klabu ya Chess iitwayo Queens of Chivhu - iliyochochewa na kupewa nguvu na Malkia wa Katwe - kusaidia wanafunzi wasichana kuboresha ujuzi wao wa kufikiri na hisabati kupitia mchezo huo. Dembure alikuwa amejifunza kucheza Mchezo huo alipokuwa mwalimu/ mwanafunzi.

“Wakati naanza mradi huu wa mchezo wa Chess ilikuwa ni dawa ya kukabiliana na matatizo yaliyokuwapo katika eneo nililokuwa nafundisha, ndoa za utotoni, mimba na kuacha shule zilikuwa nyingi sana na zilizokithiri, jambo ambalo lilinifanya nitafute namna ya kuwasaidia wasichana hawa. kujiamini na kujiondoa katika hali waliyokuwa nayo," Dembure anaiambia TRT Afrika.

Shirika la Taifa la Takwimu la Zimbabwe linasema wasichana wa mashambani wana uwezekano mara mbili zaidi wa kuolewa kabla ya miaka 18. Picha: TRT Afrika

Takwimu za Shirika la Taifa la Takwimu la Zimbabwe (Zimstat) zinaonyesha kuwa wasichana wa vijijini wana uwezekano mara mbili zaidi wa kuolewa kabla ya miaka 18 kuliko wenzao wa mijini.

Zimstat pia inabainisha kuwa 33.7% ya wasichana wenye umri wa chini ya miaka 18 tayari wameolewa, ambayo ni sawa na msichana mmoja kati ya watatu chini ya miaka 18. Kwa kulinganisha, ni 2% tu ya wavulana wanaooa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.

Zimbabwe ni miongoni mwa nchi 20 za Afrika ambako ndoa za utotoni zimekithiri.

Changamoto za ufadhili

Nchini Zimbabwe, bao bado inachukuliwa kama mchezo wa wasomi, unaochezwa zaidi katika shule za juu za nchi hiyo. Kitovu cha chess inasemekana ni sehemu za vijijini ambazo zinashughulika na masuala ya kilimo sehemu za mashambani kama Chivhu ndicho kitovu pekee. Wasichana wanaoibuka kutoka klabu ya Dembure's Queens ya Chivhu tayari wameshinda katika viwango mbalimbali vya mchezo huo wa chess huku wakishiriki na kushinda mashindano ya ndani, kitaifa na kimataifa.

Dembure anasema ufadhili wa kuwezesha wasichana wa sehemu mbalimbali katika eneo lake kuhudhuria mashindano ni changamoto kutokana na kukosekana kwa njia za kujiongezea kipato. Wazazi katika eneo hilo tayari wanapata shida ya kukutana na vikwazo vya ukosefu wa pesa kulipia elimu ya watoto wao - kwa hivyo, kuna mambo machache zaidi wanaweza kutoa kwa mchezo wa chess.

Wakati mwingine, Dembure huishia kufadhili klabu na mapato yake mwenyewe ili wasichana waweze kwenda kwenye mashindano na kupata uzoefu wa ushindani ambapo mashindano hayo hualika sehemu ambazo zina viwanja vikubwa zaidi na vingine vilivyo karibu vinakaribishwa.

Viwanja vikubwa zaidi vinakaribisha

Klabu ya Queens of Chivhu ilishinda ubingwa wa kitaifa wa Zimbabwe mwaka wa 2018. Picha: TRT Afrika

Kando na Grace, wachezaji wengine wawili kutoka Queens ya Chivhu - Lynne Chidanhire na Patricia Madziva - wanatarajiwa kusafiri kwenda Misri mwaka huu kwenye kupambania Ubingwa wa Afrika wa chess kwa Vijana. Mmoja wa wasichana hao bado hana pasipoti.

Klabu hiyo ilishinda ubingwa wa kitaifa wa Zimbabwe mnamo mwaka 2018, lakini haikuweza kuhudhuria mashindano ya Afrika nchini Misri kwa sababu ya uhaba wa kifedha. Mwaka jana, timu hiyo ilikuwa na wachezaji waliofuzu kwa michuano ya Afrika kwa Vijana ya chess nchini Ghana, lakini haikuweza kuwapeleka huko kwa kukosa ufadhili.

Mnamo 2019, mpango wa GoFundMe kwenye Twitter ulifanya mafanikio kwa kuchangisha dola 5,000 za Kimarekani chini ya saa 24 kwa timu ya wachezaji wanne ya Queens of Chivhu na kushindana katika Mashindano ya Chess ya Shule za Kiafrika katika mji mkuu wa Namibia wa Windhoek. Grace amekosa medali, akimaliza wa nne katika kikundi cha umri wake.

Michuano ya chess ya Vijana ya Afrika, kiwango cha juu zaidi barani, inatumika kama hatua ya kufuzu kwa Mashindano ya Dunia ya chess au chess yatakayofanyika mwakani kuanzia Aprili 3 hadi 25 huko Toronto, Canada.

Kwa Grace na Queens wengine wa Chivhu, changamoto zote za zamani zimesalia, lakini talanta na karama zao katika mchezo huu wenye hadhi ya kifalme imehakikisha kwamba maisha si mkwamo tena.

TRT Afrika