Yvans Conde: Mwanamitindo anayetumia bidhaa zilizotumika kama malighafi

Yvans Conde: Mwanamitindo anayetumia bidhaa zilizotumika kama malighafi

Mitindo ya mbunifu huyo imewashangaza wengi, hasa kutokana na uendelevu wake.
 Yvans Conde anatengeneza nguo kutoka kwenye bidhaa zingine kama vile mablanketi. Picha: Conde   

Na Pauline Odhiambo

Yvans Conde hakuwa na uwezo wa kununua hata kitambaa wakati anafikiria kuanza kuingia kwenye tasnia ya ubunifu wa mitindo.

Ama kwa hakika, ule usemi wa Kiswahili usemao "Kila Mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake", uliakisi nia yake thabiti ya kuzama katika ulimwengu wa uanamitindo.

"Mara kadhaa, ningebadilisha mtindo wa mavazi ya mama na dada yangu, ili kupima uwezo wangu. Huu ndio ukawa mtindo wangu," Conde anaiambia TRT Afrika.

Kama mwanamitindo anayechipukia, maono ya kijana mwenye umri wa miaka 28 hayazuiwi kwa njia yoyote na uamuzi wake wa kufahamu wa kwenda katika njia isiyokanyagwa katika tasnia ambayo mara nyingi inauza maonyesho.

Michoro yake inaweza kuwa midogo, lakini miundo yake huchota msukumo kutoka kwa viumbe vizuri na maridadi wa asili: ndege wa tausi.

Miundo mingi ya Conde imetengenezwa kutoka kwa vitambara vya 'jeans'. / Picha: Conde

Conde alipoanza kutafuta jina la chapa yake, alijikita kwenye "Tausi", ambayo ina maana ya ndege wa aina ya tausi katika lugha ya Kiswahili.

Hii ilikuwa miaka mingi baada ya kujifunza kutoka kwa bibi yake kwamba jina lake la ukoo "Conde" linatafsiriwa kwa "manyoya ya tausi" katika lugha ya asili ya Uganda.

"Tausi Conde" inaweza kusikika kama ya kuchekesha, lakini Conde alishikilia kile alichoamini kuwa kingetoa mfano wa chapa yake.

Tangu kuzinduliwa kwake mwaka wa 2017, Tausi Conde limekuwa jina la kukumbukwa kwa mtindo endelevu, linalotokana na tausi na asili.

"Nataka watu wanaovaa nguo zangu wajisikie maridadi na warembo wa kipekee kama tausi," asema.

Muundo wa Conde zimetokana na umaridadi wa ndege aina ya tausi . /Picha: Conde

Mtindo rafiki kwa mazingira

Ingawa wazo la kushikilia mtindo wa Prêt-à-porter wa Conde kama mtindo wa kimaadili ulikuwa wa bahati mbaya kama jina lake la ukoo likilingana na maono yake kwa chapa hiyo, aliamua kusalia kwenye mtindo huo hata baada ya rasilimali kutokuwa changamoto tena.

"Ninaweza kununua kitambaa kipya sasa, lakini ninachagua kuchakata vitambara. Inanivutia kwamba ninachofanya ni kizuri kwa mazingira," anaiambia TRT Afrika.

Kulingana na jukwaa la State of Matter Apparel, jukwaa ambalo linaangazia mavazi endelevu, takriban asilimia 95 ya nguo zinazotupwa zinaweza kuchakatwa. Kwa kweli, karibu asilimia 15 ya nguo zilizotupwa huchakatwa.

Bidhaa za mtindo wa haraka mara nyingi huvaliwa chini ya mara tano, hutunzwa kwa takriban siku 35, na hutoa zaidi ya asilimia 400 ya uzalishaji wa kaboni kwa kila nguo kila mwaka kuliko nguo zinazovaliwa mara 50 na kuwekwa kwa mwaka mzima.

Conde anasema wazo la kuwa sehemu ya mchakato wa kiikolojia lilichochea azimio lake la kuchangia tasnia ya mitindo ya maadili, ambayo inakadiriwa kuwa na thamani ya dola za Kimarekani bilioni 8.3 ifikapo 2025.

Kwa sasa Conde ndiye mbunifu mkuu wa chapa isiyo ya faida ya Maisha na Nisria. Picha: Conde

Kwa sasa Conde ndiye mbunifu mkuu wa chapa isiyo ya faida ya Maisha by Nisria, ambayo inajishughulisha na mitindo endelevu. Maisha inamaanisha "maisha" kwa Kiswahili.

"Kuchukua vitu vilivyotupwa na kugeuza hivi kuwa kitu cha kuvutia zaidi inalipa kwa sababu inaniruhusu kuweka maisha mapya katika kitu cha zamani," anasema Conde, ambaye anaongoza timu ya 10 inayojumuisha wasaidizi wa mitindo, washonaji nguo na wanafunzi.

"Kulingana na msimu, tunaunda nguo kutoka kwa blanketi, mapazia, au vitambaa vingine vilivyotumika ambavyo vinafaa kwa hali ya hewa."

Chapa mpya ya Hayat Collection uliundwa ili kuunga mkono kadhia ya Palestina baada ya mashambulizi ya kimbari ya Israeli huko Gaza.

"Hayat inamaanisha maisha katika lugha ya Kiarabu, na miundo katika chapa hio inaonyehsa umuhimu wa uchakato huku pia ikiangazia uzuri wa mtindo wa jadi wa Kiarabu-Palestina," Conde anaeleza.

Chapa hio pia inamtukuza mmoja wa waanzilishi-wenza wa Maisha, mtu wa asili ya Palestina ambaye aliaga hivi majuzi.

Conde anaongoza timu ya 10 inayojumuisha wasaidizi wa mitindo, washonaji nguo na wanafunzi. Picha: Conde

Kielelezo kwa Wengi

Wanafunzi wengi katika timu ya Conde wanatoka katika jamii za ndani, ikiwa ni pamoja na baadhi ya watu wasizojiweza.

"Wanafunzi bora huingizwa kwenye timu ya wabunifu, na mara nyingi wao ndio wenye ujuzi wa ushonaji," anasema.

Maisha by Nisria pia inasaidia jamii kupitia mpango wa chakula kwa wanafunzi wachanga katika shule za mitaa.

Conde anasema shauku yake ya kuunga mkono wapenda mitindo wachanga inatokana na tajriba yake shuleni, akikumbuka aliposhiriki katika kategoria ya wanafunzi katika Tuzo za Kenya Fashio Awards.

Conde mara nyingi hushirikiana na wataalamu wengine wa mitindo katika kubuni chapa mpya. Picha: Conde

"Nilisomea uanamitindo katika Chuo Kikuu cha Kenyatta kabla ya kuchukua mapumziko ili kuanza kufanya kazi na kujifunza zaidi kuhusu mitindo katika ulimwengu halisi," anaambia TRT Afrika.

"Kuonyesha miundo yangu kwenye hafla tofauti za mitindo kulinisaidia kuteka hisia za watu polepole."

Ushauri wake kwa wabunifu wanaotaka ni kuamini katika nguvu ya ushirikiano.

"Usiogope kuungana na wapiga picha, wasanii wa vipodozi na wabunifu wengine wa mitindo kwa sababu ni gharama ya chini kuunda chapa kwa njia hiyo," anasema.

"Chagua tu utaalam na uzingatie kujenga chapa yako. Hatimaye pesa zitakuja."

TRT Afrika