Wasanii wa kiafrika akiwemo Davido ni miongoni mwa watakaotuzwa pamoja na mastaa wengine / Picha: Reuters

Makala ya 66 ya sherehe ya tuzo za kifahari zaidi za muziki Grammy inaashiria mwaka wa kihistoria kwa wasanii wa kiafrika watakaotuzwa miongoni mwa mastaa wengine.

Wasanii hao watagombania tuzo ya maonyesho bora ya muziki wa kiafrika ambacho ni mojawapo ya vitengo vitatu vipya vilivyoongezwa kwenye Grammy, mwaka 2024.

Licha ya atakayeshinda kitengo hicho, tuzo hiyo, ya GRAMMY kwa Utendaji bora wa muziki Afrika, wote watakuwa wakiweka historia katika mchakato kwani tuzo hiyo inaonekana kama mafanikio kwa sekta ya muziki barani Afrika.

"Kukabidhi muziki wa Kiafrika kitengo chake kitaangazia na kusherehekea utofauti na utajiri wa Afrika," Shawn Thwaites, meneja wa miradi katika taasisi 'Recording Academy,' alisema juu ya kitengo kipya. "Hii ni hatua kubwa mbele!"

Nyota wa Afrobeats kutoka Nigeria Burna Boy, Asake, Davido, na Ayra Star wote wamepata uteuzi kuwania tuzo hiyo.

Wasanii hao wanawania tuzo kwa nyimbo zao :

"Amapiano"- ASAKE na Olamide

"City Boys" - Burna Boy

"UNAVAILABLE" - Davido na Musa Keys

"Rush" - Ayra Starr

"Water" - Tyla

Kulingana na waandalizi, 'The Recording Academy ' kuanzishwa kwa kitengo hicho pia kulikuja ili kukabiliana na "ukosoaji kwamba tuzo hizo hazikuashiria mageuzi katika sekta ya muziki na hazikuonyesha usawa."

TRT Afrika