Shirika la anga za juu la Kenya, Kenya Space Agency, linasema kurushwa kwa setilaiti ya kwanza ya anga za juu nchini humo kuhairishwa hadi Jumatano tarehe 12 Aprili 'Taifa 1' inayomaanisha iliratibiwa kutumwa angani Jumanne na roketi za kampuni ya SpaceX saa 3:44 asubuhi ( EAT).
Uzinduzi huo utafanywa ndani ya roketi ya FALCON-9, kutoka kambi ya Vandernberg huko California, Marekani.
Kulingana na taarifa ya Shirika la Anga za Juu la Kenya, kampuni ya SpaceX inasema kuna "hali mbaya ya upepo wa hali ya juu ambayo inaweza kuathiri njia ya kuruka ya roketi."
Setilaiti iliyofungwa kamera itafuatilia hali ya hewa, mafuriko, hali ya mazao na athari za mabadiliko ya hali ya hewa nchini Kenya.
Shirika la Anga za Juu la Kenya linasema kucheleweshwa kwa uzinduzi wa ‘Taifa 1’ pia kutaathiri mataifa mengine ambayo yanatumia chombo hicho cha usafiri.