Shirika la Chakula Duniani , WFP, linasema nchi za Afrika ni kati ya nchi 48, zenye idadi ya watu wanaohitaji msaada wa chakula.
Hii imeripotiwa kuwa ongezeko ya asili mia 10 tangu mwaka jana.
Ripoti ya mpya inayoangazia hali ya chakula duniani, imetolewa na mashirika 16 ya kimataifa ikiwemo WFP. Ripoti hiyo, inaonyesha kuwa hali ya njaa imeongezeka katika nchi kama Sudan, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Burundi na Ethiopia.
"Nchi tisa zinakabiliwa na kudorora kwa hali ya chakula tangu 2022, miongoni mwao ni Sudan yenye ongezeko la watu milioni 8.6, na Somalia na Burundi kila moja ikiwa na takriban ongezeko la watu milioni 1," ripoti hiyo imesema.
Katika kanda ya Afrika Mashariki, ripoti inaonyesha kuwa idadi ya walioathrika na njaa inasababishwa na vita nchini Sudan, ambapo karibu watu milioni 3.5 wamelazimika kuhama tangu Aprili.
Vita nchini Sudan viilianza tarehe 15 Aprili kati ya jeshi la Sudan na kikundi cha Rapid Support Forces, na hadi sasa hakuna suluhisho lililopatikana.
Hali kali ya hewa ndio chanzo kikuu nchini Kenya, Somalia na Uganda.
Migogoro na kutokuwa na usalama ni kichocheo kikuu nchini Sudan, na ni jambo muhimu katika Somalia na Sudan Kusini.
Nchini Ethiopia, migogoro na ukosefu wa usalama ni chanzo kikuu kaskazini, na hali ya hewa iliyokithiri katika maeneo mengine.