Na Kudra Maliro
Tamasha la mwaka huu la Guérouwal nchini Niger, ambalo kwa kawaida huleta pamoja koo za Fulani zilizoenea katika nchi za Afrika Magharibi na Kati zikiwemo Burkina Faso, Nigeria, Chad, Cameroon na Jamhuri ya Afrika ya Kati, limeghairishwa.
Wafulani kimsingi ni wafugaji wa ng'ombe wanaoishi katika eneo pana la kijiografia kutoka bahari ya Atlantiki upande wa magharibi hadi Ziwa Chad katikati mwa Afrika.
Lakini zaidi ni kundi la Wodaabé la Fulani ambao wamedumisha maisha yao ya kuhamahama kama wafugaji na wafanyabiashara.
Ndio nguvu inayoongoza ya Guérouwal ambayo inamaanisha "gwaride la vijana au tamasha la uzuri" katika lugha ya Fulani.
Ni sherehe ya kitamaduni ya kuheshimu urembo, umaridadi na urithi Ambayo hufanyika kuashiria kuanza kwa msimu wa mvua kila mwaka. Sherehe hizo ni pamoja na mbio za ngamia pia zinapambwa na nyimbo na densi.
Lakini matukio makubwa yameahirishwa mwaka huu. "Hatutafanya Guérouwal mwaka huu kwa sababu ya matatizo ya kifedha. Tamasha zitaandaliwa katika jumuiya ndogo," Aboubacar Yacouba Maiga, mkuu wa kitengo cha tamasha na maonyesho ya biashara katika Wizara ya Utamaduni, aliiambia TRT Afrika.
Wakati wa sherehe hizo, watu wa Peulhs au Fulani hufanya mashindano ya uchumba ambapo vijana wa kiume huvaa mavazi yao ya kifahari, kujipodoa na kufanya gwaride mbele ya wanawake, ambao huchagua mchumba wao.
"Wanawake pia huchaguliwa na wanaume, lakini mwanamke anapaswa kukubali. Kwa sababu kwa Wabororo (ukoo wa Fulani), hakuna ndoa ya kulazimishwa, hakuna ndoa ya kupanga, ni mwanamke anayechagua mwanamume," anaongeza Bw Yacouba Maiga. .
Mshindi anapata haki ya kuoa mwanamke wa chaguo lake, kwa makubaliano ya familia yake.
Ni fursa ya kujumuika pamoja, kubadilishana mawazo na kuimarisha uhusiano wa kijamii na familia. Tukio hili ni kivutio kikubwa kwa watalii ambao wana hamu ya kugundua utamaduni huu wa kuvutia wa mababu.
Mashirika kadhaa ya usafiri hutoa vifurushi vya utalii kwa watu wanaopenda kuhudhuria tamasha na kufurahia uzoefu usiosahaulika. Wizara ya utamaduni ya Niger inaunga mkono tamasha hilo na kulikuza kama ishara ya utofauti wa kitamaduni na umoja wa kitaifa.
"Guérouwal ni tamasha la kitamaduni la kila mwaka ambalo hufanyika kwa kawaida, kama unavyojua, ni tamasha la kuhamahama ambalo kwa ujumla hufanyika karibu na shimo la kumwagilia.