Na Charles Mgbolu
Bruce Lee leo hii katika Karne hii anasifiwa kwa kukuza tasnia ya filamu za nchini China nchi ambayo ina mji maarufu sana huitwao Hong Kong na kusaidia kubadilisha mitazamo Wachina waliokuwa wanatazama sana filamu za Marekani.
Mnamo Julai 20, 1973, Bruce Lee, msanii wa Kichina ambaye amefahamika na filamu zake zenye ngumi maarufu kama “Martial Arts” ambaye filamu zake ziliteka na zilisambaa duniani kote, aliaga dunia kwa kusikitisha baada ya kuathiriwa na dawa aliyokuwa amemeza ili kutibu maumivu ya kichwa.
Bruce lee ambaye ni Mzaliwa wa San Francisco aliyezaliwa Novemba 27, 1940, Lee, 32, alielezwa na vyombo vya habari, na wasanii wengine wa ngumi kuwa msanii wa filamu za maigizo ya ngumi mwenye ushawishi mkubwa wa wakati wote na mtu maarufu ya utamaduni wa Kichina katika karne ya 20 ambaye aliziba pengo la Nchi zz Mashariki, Magharibi Na Asia ya Kati kutokana na filamu zake kusambaa sana katika maeneo hayo.
Anasifiwa kwa kukuza tasnia ya sinema ya Hong Kong na kusaidia kubadilisha desturi ya Wachina walivyoonyeshwa katika filamu za Amerika na baadae kupenda desturi ya filamu zao.
Barani Afrika, kumbukumbu ya miaka 50 ya kifo chake ni chanzo kikuu cha shauku kwa watengenezaji filamu ambao walikua wakivutiwa na tabia yake ya mapigo yenye nguvu kwenye televisheni.
'Kubwa kuliko maisha'
‘’Siku zote nilipenda kujiamini kwake katika matukio yake. Alikuwa mkubwa kuliko maisha, na haikuwahi kuhisi kama angepoteza maisha." Anasema Matthew Chan-Piu, Mtayarishaji filamu wa Uganda ambaye alikua akimtazama sana Bruce Lee.
‘’Kinachonivutia zaidi ni pale anapoingia kwenye kile kisiwa na kuanza kucheza na chatu; ndio, alikuwa wa ajabu sana,'' anaiambia TRT Afrika. Haliru Uba Salihu Nakande, shabiki mwingine kutoka kaskazini mwa Nigeria, alielezea Bruce Lee kama mchawi. ‘’Ujuzi wake wa karate ulikuwa wa kusisimua. Alicheza kila jukumu alilopewa kwenye filamu husika kikamilifu na aliuvaa uhusika ipasavyo. Bado napenda filamu zake,’’ anasema. ‘’Lakini kwa bahati mbaya, filamu zake nyingi zinatoweka katika jamii yetu kutokana na kushamiri kwa tasnia ya filamu nchi mbalimbali na mabadiliko ya nyakati ambapo sasa filamu za kisasa zenye utandawazi zimeshamiri’’ alieleza Nakande.
Tai Chi na ndondi ndiyo mapigo yaliyomtambulisha Bruce Lee alitambulishwa kwa tasnia ya filamu ya China kama muigizaji mwenye uzoefu mkubwa kutokana na namna yake ya kipekee ya uigizaji wake.
Mnamo Mwaka 1959 Bruce Lee alihamia Seattle, na mnamo 1961, alijiunga na Chuo Kikuu cha Washington. Wakati huo nchini Marekani ndipo alipoanza kufikiria kupata pesa kwa kufundisha sanaa ya mapigano. Wanafunzi wake ni pamoja na Chuck Norris na marehemu Sharon Tate, wote walikuwa waigizaji mashuhuri wa Marekani.
Katika miaka ya 1970, filamu zake za Hong Kong na Hollywood zilizotayarishwa ziliinua filamu zinazotumia mapigano ya kutumia “Martia Arts” ambapo kilikuza na Kuongeza umaarufu na sifa, na hivyo kuzua shauku ya nchi za Magharibi katika kujifunza tasnia Hiyo ya kuigiza ya China.
Mpangilio na Mwelekeo wa sauti za filamu zake ziliathiri sana na kubadilisha sanaa ya kichina na filamu za karate duniani kote. ‘’Kujenga na Kumtengeneza Mwingizaji mwingine kama yeye katika filamu ambayo ingevuka vizazi na vizazi na kuishi miaka mingi itakuwa vigumu,’’ anasema Chan-piu. Mmoja wa wadau Katika tasnia ya wa sinema
‘’Kizazi hiki cha vijana cha wapenda filamu hawana subira sana na kinakua kwa haraka sana. Hawachukui muda wao kufikiria waigizaji wa kina wa sinema, Njia Pekee ni kukutana na wazalishaji ambao wanaweza kurithi mapigano ya Bruce Lee,’’ Chan-Piu aliongeza.
Kumbukumbu ya miaka 50 ya kifo chake inaadhimishwa kwa umaridadi mkubwa kote ulimwenguni, huku Jumba la Makumbusho la Urithi la Hong Kong likiandaa maonyesho na kambi ya siku 5 ya watoto majira ya kiangazi, huku jumba la makumbusho la Pico House huko Los Angeles likizindua sanamu yenye ukubwa wa maisha ya Bruce Lee ambao itatumika kama kivutio Cha Utalii.