Mamlaka za Zimbabwe zinasema ''hazina nafasi yoyote'' katika vita dhidi ya dawa za kulevya. Picha: TRT Afrika

Rufaro Machingura alikuwa nyota wa soka wa Zimbabwe - mfano wa kuigwa kwa vijana na "mshambulizi bora", taji alilopewa na rais wa zamani Robert Mugabe. Alifahamika zaidi nchini humo, kama mchezaji ambaye alifunga bao pekee na kuiongoza timu ya taifa, ‘Mighty Warriors’, kutwaa ubingwa wa baraza la vyama vya soka kusini mwa Afrika la Wanawake mwaka 2011 nchini Afrika Kusini.

Alikufa mwezi January mwaka huu, akiwa mdogo, na umri wa miaka 31 pekee, baada ya kukiri matumizi mabaya ya dawa za kulevya ambazo hatimaye ziliharibu kazi na afya yake.

Hadithi ya Rufaro ni mfano wa kinachowakumba baadhi ya vijana nchini Zimbabwe.

Kuongezeka kwa matumizi ya madawa ya kulevya ambayo yanaharibu maisha ya watu binafsi na familia.

Hadithi za watu maarufu, kama vile Rufaro, na mwimbaji maarufu wa Zimbabwe Tinashe Gonzara, aliyeshinda tuzo, huwa vinajaza vichwa vya habari mara kwa mara. Maelfu ya wengine wengi huishia kuwa takwimu tu katika rekodi za serikali.

Utafiti wa matumizi ya dawa za kulevya vimehusisha matumizi yake na kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira kwa vijana na matumizi ya nchi ya Zimbabwe kama njia ya kupitisha dawa kama vile kokeni kuelekea nchi zingine Afrika Kusini.

Vita ya Bure

Kwa miaka mingi, mashirika ya kutekeleza sheria nchini Zimbabwe yamezindua mipango mingi ya kujaribu kupunguza hatari ya uuzaji wa madawa ya kulevya , ikiwa ni pamoja na kuweka vizuizi vya barabarani, lakini hii haijafua dafu.

Vita dhidi ya mihadarati ni shida Zimbabwe
Kituo cha Dawa

Ulanguzi wa dawa za kulevya umekithiri kote nchini Zimbabwe, hasa kupitia mipaka yake na Afrika Kusini, Zambia na Msumbiji. Hizi zimeibuka kama vyanzo vipya vya dawa halali na isiyo halali ambazo zote hutumika vibaya.

Kwa mfano kuna dawa inayoitwa bronclear ambayo madaktari hushauri kutumika kutibu kikohozi na homa , lakini watu huitumia vibaya kwa kukunywa zaidi ya kiwango kinachohitajika.

Zingine ambazo zinatumika vibaya licha ya kuwa dawa halali ni pamoja na Diazepam, Ketamine na Pethidine, Morphine na Fentanyl.

Utekelezaji wa sheria wa Zimbabwe mara nyingi hupekua magari na wasafiri kutafuta dawa za kulevya. Picha: TRT Afrika

Ripoti za vyombo vya habari nchini Zimbabwe zinaonyesha kuwa kwa miaka mingi, zaidi ya wanawake 50 wamekamatwa kwa ulanguzi wa dawa za kulevya. Ripoti moja ilisema kuwa wanawake sita wa Zimbabwe walifariki walipomeza dawa walizokuwa wakisafirisha ili kukwepa kukamatwa.

Kando na dawa zinazoagizwa kutoka nje, wenyeji pia wamejaa sokoni na dawa zao za bei nafuu, zinazolewesha sana. Hii ni kama dawa inayoitwa musombodiya, kinywaji kisicho na rangi kilichotengenezwa na kemikali ya ethanol na nembo za poda zinazotengenezwa na husambazwa hasa kwenye vituo vya mabasi na katika maeneo ya makaazi duni.

Ripoti zingine zaonyesha kuwa vijana huchukua nepi za watoto na bidhaa za kemikali , wanazichemsha na kuvuta mivuke kama vileo.

"Watumiaji wa dawa za kulevya wanaweza kuchukua chochote wanachofikiri kitawafanya wafurahi au kutuliza na visa vya saikolojia ya kikaboni vinaongezeka,”anasema Dkt. Johannes Marisa, rais wa rais wa muungano wa madaktari binafsi wa madaktari na meno wa Zimbabwe.

Anaongeza kuwa kuna haja ya kuwa na vituo vingi vya kurekebisha tabia nchini ili kupunguza idadi ya waathirika wa dawa za kulevya wanaohitaji kurekebishwa” Marisa anasema.

Polisi wa Jamhuri ya Zimbabwe, mwezi Januari mwaka huu, walianzisha operesheni ya kitaifa inayoitwa "Kupinga madawa ya kulevya na vitu haramu", ambayo ilikuwa imenasa washukiwa na watumiaji wa dawa za kulevya 1,903 kufikia Februari 10.

Waziri wa mambo ya ndani na urithi wa utamaduni Kazembe Kazembe anasema pia kuna mipango ya kuwasaka wauzaji wakubwa wa madawa ya kulevya .

“Tunasema hapana kwa matumizi ya madawa ya kulevya na madawa ya kulevya. Polisi na wanasiasa ni miongoni mwa washukiwa, na watawajibishwa pia,” anaongezea.

TRT Afrika