Takriban watu milioni sita na laki sita walijiandikisha kupiga kura katika taifa hilo lenye idadi ya takriban watu milioni 15.
Akipiga kura yake katika mji alikozaliwa wa Kwekwe, katikati mwa Zimbabwe, rais wa sasa Emmerson Mnangagwa anayegomea kiti kwa awamu ya pili, aliwaambia waandishi wa habari,
"Kama nadhani sitachukua, basi nitakuwa mjinga."
Nelson Chamisa mgombea mwingine anaonekana kama mpinzani mkuu wa rais Mnangangwa.
Matokeo ya ubunge yanatarajiwa kuanza kutangazwa kufikia Alhamisi asubuhi. Matokeo ya urais yanatarajiwa kuja baadaye, ingawa ni ndani ya siku tano.
Ili kushinda urais, mgombea lazima apate zaidi ya 50% ya kura.
Ikiwa hakuna mshindi wa moja kwa moja, marudio ya uchaguzi yatafanywa kati ya wagombea wawili wa juu yatafanyika Oktoba tarehe 2.
Wagombea wa kura za udiwani wanahitaji puta wingi wa kura zilizopigwa ili kutangazwa washindi