Yanga kuchuana na Al Ahly. Picha: Yanga 

Licha ya kuchuana na mpinzani maarufu, hata hivyo, tayari Young Africans, 'Yanga' ya Tanzania imetua robo fainali ya mashindano ya klabu bora Afrika na kujiunga na Asec Mimosas kutoka Ivory Coast, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambao pia ni mabingwa wa Ligi ya soka ya Afrika, Petro de Luanda ya Angola, Mabingwa wa zamani wa Afrika na wanafainali wa Kombe la Dunia wa vilabu FIFA, TP Mazembe.

Hata hivyo pande hizo zitawania kuwa kiongozi wa kundi Yanga wamejikusanyia pointi 8, nao Al Ahly, viongozi wa kundi hilo, wakiwa na pointi tisa, pointi moja zaidi ya Yanga.

Kikosi cha Yanga kitaingia uwanjani kuchuana na Al Ahly kwenye mechi itakayochezwa katika uwanja wa Kimataifa wa Cairo, nchini Misri, siku ya Ijumaa.

Yanga watavaana na Mabingwa watetezi wa Misri, Al Ahly wanaolenga kutetea taji lao baada ya kuifunga Medeama ya Ghana 1-0 na kufuzu kwa hatua ya kusisimua ya mtoano wa kombe hilo.

TRT Afrika na mashirika ya habari