Visa vya Uviko 19 vinaendela kuripotiwa sehemu tofauti barani Afrika / Picha: Reuters

Shirka la Afya Duniani, WHO linaonya kuwa magonjwa ya mfumo wa upumuaji kutoka Uviko 19, mafua na vimelea vingine vya magonjwa yamekuwa yakiongezeka katika nchi nyingi kwa wiki kadhaa, na hali hii inatarajiwa kuendelea.

"Kama watu binafsi hakikisha umepima na kutafuta huduma inapohitajika kwa sababu matibabu ya Uviko19, yanaweza kuzuia ugonjwa mbaya na kifo," Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom ameonya.

"Endelea kutumia barakoa, hakikisha hewa safi ya kutosha mahali ulipo na uhakikishe kuwa wewe na wapendwa wako mmempata chanjo zinazohitajika za Uviko19.

Wataalamu wa afya wanasema takriban nusu ya waathiriwa wa Uviko19 katika nchi za Kiafrika wanaripoti angalau dalili moja inayoendelea ambayo haiwezi kuelezewa na hali zingine za matibabu.

Watafiti wanasema uchovu na dalili zingine zinazoendelea tayari zinaathiri ubora wa maisha ya watu na zinaweza kudhoofisha uwezo wao wa kufanya kazi, na kuwafanya wawe katika hatari kupata maambukizi mapya kwa urahisi.

Ingawa sio tishio la kimataifa tena bado Uviko 19 inaendelea kuripotiwa katika sehemu tofauti barani Afrika.

Kulingana na Vituo vya kudhibiti Magonjwa Afrika, Africa CDC tangu janga la Uviko19 kuanza visa 12,216,748 vimeripotiwa barani Afrika hadi sasa,

Eneo la Kusini mwa Afrika limeripoti visa zaidi.

WHO bado inasaidia serikali kupata uwezo wa kufanya vipimo vya tishio za afya zizazohusisha kupumua.

" Serikali zinafaa kuhakikisha wananchi wanapata vipimo vya kuaminika, matibabu na chanjo, haswa kwa wale ambao wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa sana," Adhanom ameongezea.

Mwaka huu Rwanda imeanza kujitayarisha kuzalisha chanjo aina tofauti mkiwemo chanjo dhidi ya Uviko 19. BioNTech kamouni ya Chanjo kutoka Ujerumani kimefungua kituo huko Kigali, Rwanda..

Kituo hiki kimeundwa kwa ajili ya kutengeneza chanjo kwa ajili ya matumizi ndani ya bara la Afrika.

Rwanda sasa itaweza kutoa hadi dozi milioni 50 za bidhaa kila mwaka .

TRT Afrika