Waziri Mkuu wa Somalia Hamza Abdi Barre amemfuta kazi Waziri wa Fedha Elmi Mahmud Nur.
Kufutwa kwa Nur kunakuja siku chache baada ya kuwasimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Mohamed Abdirahman Anas na mkurugenzi wa mapato kwa madai ya utovu wa nidhamu.
Bihi Egeh, ambaye alikuwa waziri wa ajira na masuala ya kijamii, sasa ameteuliwa kuwa waziri mpya wa fedha.
Kufutwa kazi kwa Nur kuliwasilishwa kupitia ofisi ya Waziri Mkuu wa Somalia siku ya Jumamosi.
Akichukua jukumu lake mpya, Egeh alisema kwenye Twitter: "Kwa kweli nimepokea kwa heshima na unyenyekevu jukumu la kuhudumu kama Waziri wa Fedha wa Serikali ya Shirikisho la Somalia."
" Asante waziri mkuu Hamza Abdi Barre kwa imani yako kwangu (kwa mara nyingine tena) na ninashukuru kwa fursa ya kulitumikia taifa letu katika kipindi hiki kigumu."
Pia akitumia Twitter, waziri aliyefutwa kazi Mahmud Nur alisema:
"Ninajivunia kwa kuhudumu kama Waziri wa Fedha wa Somalia. Bado tupo katika mustakbali wa kupata afueni ya deni letu la kimataifa, ninapoondoka ofisini. Tunaweza kufikia lengo hili tukiwa na utawala bora, kuteua wafanyakazi wenye ujuzi na kuzingatia mapato ya ndani. Namtakia mafanikio waziri mpya.”
Nur, alibatilisha uamuzi wake Alhamisi, Julai 6 wa kuwafuta kazi Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na mkurugenzi wa mapato. Alielezea kubadili uamuzi wake katika barua ya Julai 7.
Asante PM @HamzaAbdiBarre kwa imani yako kwangu (kwa mara nyingine tena) na ninashukuru kwa fursa ya kulitumikia taifa letu katika kipindi hiki kigumu."