Wavuvi wa Cameroon wakikumbatia mitumbwi ya chupa za plastiki

Wavuvi wa Cameroon wakikumbatia mitumbwi ya chupa za plastiki

Shirikal la NGO la Madiba and Nature hutumia chupa 1000 kutengeneza mtumbwi wa wavuvi.
Cameroon inazalisha takriban tani 600,000 za plastiki kwa mwaka. Picha: TRT Afrika

Na Anne Nzouankeu

TRT AFRIKA,Yaoundé

Katika ufuo wa Londji nchini Cameroon, kando ya mitumbwi ya kitamaduni ya mbao, sasa kuna mitumbwi iliyotengenezwa kwa chupa za plastiki.

Mvuvi Camille Dimale amekuwa akitumia mtumbwi huu wa chupa za plastiki kwa miaka miwili, na anasema ameridhika.

"Ni nyepesi na ni rahisi kwangu kutumia kwa sababu wakati mwingine naenda kuvua peke yangu. Hivyo naweza kuibeba kirahisi, kuipeleka majini, kuisogeza bila kuhitaji msaada. Haiharibiki kirahisi hivyo," Dimale anasema.

"Inafaidi zaidi kiuchumi na inadumu zaidi. Siogopi kwamba itavuja au kupasuka. Ni kweli inafanya kazi nzuri zaidi, "anaelezea Dimale.

Wavuvi wanasema mitumbwi ya chupa za plastiki ni rahisi kutumia. Picha: TRT Afrika

Cameroon inazalisha takriban tani milioni sita za taka kila mwaka, ikiwa ni pamoja na tani 600,000 za plastiki.

Baadhi ya taka huchakatwa tena, lakini zingine, kama vile plastiki ambazo haziozi, hutupwa ovyo , na kuchafua mazingira na maji.

Shirika lisilo la kisereikali la Madiba and Nature waliamua kupunguza uchafuzi huu kwa kuchakata tena. Hukusanya chupa hizi, kuzisafisha, kuzifunga pamoja, kutengeneza mitumbwi na kuwapa wavuvi.

Mkuu wa NGO, Ismaël Essomè, mhandisi wa usimamizi wa mazingira, anaelezea kuwa alikuwa na wazo hili alipokuwa akitafuta suluhisho la kusafisha fukwe huku akiwasaidia wavuvi.

Usafishaji wa chupa za plastiki husaidia kuokoa mazingira. Picha: TRT Afrika

"Madiba na Nature waliamua kutengeneza mitumbwi kwa chupa za plastiki kusaidia uvuvi, kwa sababu uvuvi ni moja ya shughuli kuu za kiuchumi nchini Cameroon," alisema.

''Mtumbwi unaotengenezwa kwa chupa za plastiki ni wa bei nafuu, kuliko mitumbwi ya kawaida iliyotengenezwa kwa mbao, rahisi kutunza na inaruhusu mvuvi kuhamia sehemu ambazo hawezi kufika kwa mitumbwi ya kawaida," Essomè anaongeza.

Madiba na Nature wanasema inakusanya takriban chupa 3,500 kwa mwezi. Picha: TRT Afrika

NGO hiyo inasema inakusanya takriban tani tatu hadi tano za chupa za plastiki kila mwezi. Sehemu yake hutumiwa kutengeneza mitumbwi, sehemu nyingine inauzwa kwa washirika wengine wa kuchakata.

TRT Afrika