Wapiga Ngoma: Ishara ya Nguvu na Fahari kwa Burundi

Wapiga Ngoma: Ishara ya Nguvu na Fahari kwa Burundi

Nguo za rangi ya bendera ya taifa la Burundi, cheni, na ngoma za kichwa huvaliwa kuheshimu taifa wakati wa sherehe muhimu sana za kitaifa.

Oscar Nshirimimana, ambaye sasa ana umri wa miaka 46, alianza kufanya kazi kama mpiga ngoma akiwa na miaka 16, muda mfupi baada ya baba yake, mpiga ngoma kibiashara, kuhamia eneo la Gishora.

‘’Wacheza ngoma 37 chini ya uelekezi wangu wana umri wa kuanzia saba hadi themanini. Pia, kuna mzee wa ngoma ambaye hana meno tena mdomoni." kwa mujibu wa Oscar Nshirimana katika mahojiano na TRT Afrika.

Wapiga ngoma wengi walijifunza ufundi wao kutoka kwa mababu zao. Sherehe zisizo za kawaida nchini Burundi huangazia uchezaji wa ngoma hizi. Ngoma hazifai kutumika wakati wa sherehe za harusi au mazishi.

Amani Fest Burundi | Picha: Amani Fest

‘’Tunapiga ngoma wakati wa sherehe za uhuru wa Burundi na tunapo watembelea wakuu wa nchi, na pia tumeombwa kutumbuiza katika sherehe nyingi duniani’’ anasema Bw. Nshirimimana.

Kama zamani, taaluma ya mpiga ngoma inaweza kupitishwa kutoka kwa baba hadi mwana. Na ngoma hio haiwezi kuchezwa na wanawake.

Mila hutumika kama kuhalalisha katazo hili.

Kitu kama ngoma kitamaduni hufikiriwa kama aina ya taswira ya mwili wa mwanamke, na inaaminika kuwa mwanamke hawezi kucheza na mwili wake mwenyewe.

Wenyeji wanasemaje

Amani Fest Burundi | Picha: Amani Fest

Nyimbo za vikundi vya wapiga ngoma, ziwe za kielimu au za kitaaluma, zinaheshimu na kukumbuka historia ya Burundi na ushujaa wa wafalme.

Raia kadhaa wa Burundi waliohojiwa na TRT Afrika walionyesha kujivunia jinsi wapiga ngoma walivyokuwa wakiitangaza Burundi katika ulimwengu wa nje kwa kuvalia nguo, kupaka rangi ngoma na kuvaa mikufu yenye sura ya nchi hiyo.

‘’Kutokana na ukaribu wa mji wangu na wilaya ya Gishora, nimelifahamu kundi hili tangu nikiwa na umri wa miaka kumi.’’ Asema Felix Kwizera.

Kwizera anadai kuwa ‘’wapiga ngoma hao kutoka Gishora wanawakilisha nembo ya utamaduni wa Burundi, hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba ngoma za Burundi ni Eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO’’.

Serikali ya Burundi imezuia unyonyaji wa ngoma zake katika ngazi ya kitaifa na kimataifa tangu 2017 ili kulinda ngoma za nchi hii, ambazo zimeorodheshwa kama mali isiyoonekana ya kitamaduni na UNESCO.

Amani Fest Burundi | Picha: Amani Fest

‘’Wapiga ngoma wa Gishora ni fahari ya Burundi’’, kulingana na Ezéchiel Nibigira, Waziri wa Utamaduni wa Burundi, aliongezea kuwa ‘’ Serikali itawasaidia wapiga ngoma ikibidi’’.

‘’Wageni wengi huja Burundi ili kuwatazama tu wapiga ngoma hawa, na wanaipenda. Tutazindua mradi wa kupiga ngoma kwa ajili ya watalii ili kuwavutia nchini Burundi’’ anaongezea Nibigira.

TRT Afrika