Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, ametangaza kuwa wanajeshi wa Ufaransa wataanza kuondoka nchini humo kuanzia mwezi wa Januari 2025. Alitoa tangazo hilo Jumanne katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka kwa taifa.
"Tunaweza kujivunia jeshi letu, ambalo limeimarika ipasavyo. Ni katika muktadha huu ambapo tumeamua uondoaji wa pamoja na uliopangwa wa vikosi vya Ufaransa nchini nchini Ivory Coast" alisema, akiongeza kuwa kambi ya Kikosi cha 43 cha Wanamaji wa Baharini huko Port Bouet itarejeshwa kwa wanajeshi wa nchi hiyo.
Kikosi cha 43 cha Wanajeshi wa Wanamaji ni kikosi cha wanajeshi wa baharini kilichopo Port Bouet, kusini mashariki mwa Abidjan.
Hatua hiyo inafuatia maamuzi sawa katika nchi za Mali, Burkina Faso na Niger, ambako serikali zimepinga ushawishi wa Ufaransa, zikieleza wasiwasi kuhusu uhuru wa kujitawala.
Uondoaji huo unadhihirisha kuongezeka kwa hisia za kupinga ushawishi wa Ufaransa katika sehemu mbalimbali za Afrika Magharibi zikichochewa na madai ya kutoridhika na jukumu la Ufaransa katika masuala ya usalama na utawala wa kikanda.