Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby Itno alitembelea eneo hilo mnamo Oktoba 28, 2024 ili kutoa heshima kwa wanajeshi waliouawa. / Picha: Reuters

Shambulio baya dhidi ya kambi ya kijeshi katika mkoa wa Lac nchini Chad limesababisha vifo vya wanajeshi 40, kulingana na taarifa ya ofisi ya rais wa Chad.

Taarifa kutoka kwa ofisi ya rais inabainisha kuwa shambulio hilo "liligharimu maisha ya takriban wanajeshi arobaini."

Shambulio hilo lilifanyika Jumapili usiku, likilenga kambi ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika eneo la Barkaram la Lac, karibu na Ngouboua, mji ulioko karibu kilomita 480 (maili 298) kaskazini magharibi mwa mji mkuu N'Djamena.

Rais Mahamat Idriss Deby Itno alitembelea eneo hilo siku ya Jumatatu kutoa heshima kwa wanajeshi waliofariki na kuwapa pole waliojeruhiwa.

TRT Afrika